Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), kimeiomba Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa inayoongozwa na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward
Lowassa kuunda kamati ndogo kuchunguza uhusiano kati ya Tanzania na
Rwanda.
Chama hicho kimetoa ushauri huo baada ya baadhi ya
vyombo vya habari nchini Rwanda kuripoti kuwa, viongozi wa Chama cha
Upinzani cha Rwanda National Congress (RNC) na waasi dhidi ya Serikali
ya nchi hiyo (FDLR) walifanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete jijini
Dar es Salaam.
Hata hivyo, taarifa hizo zilizoandikwa na gazeti
la News of Rwanda ambalo linatajwa kuwa mshirika mkubwa wa Serikali ya
nchi hiyo, takriban wiki mbili zilizopita, zilikanushwa na Ubalozi wa
Tanzania nchini Rwanda ambao ulifafanua kuwa tarehe iliyotajwa Rais
Kikwete hakuwapo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa chama hicho, Ezekiel Wenje alisema kamati
hiyo inatakiwa kuchunguza taarifa hizo kwa sababu zinaweza kukwamisha
juhudi za kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili.
“Mbali na kuomba Kamati ya Lowassa kuchunguza, pia
tunaziomba mamlaka husika kuchunguza mchakato mzima wa utoaji wa hati
za kusafiria ili kuhakikisha jina la Tanzania halitumiki vibaya,”
alisema Wenje.
Alisema kuwa kuna haja ya Serikali kueleza msimamo
wake kwa sababu Chama cha RDI tayari kimeshaeleza nia yake ya kuung’oa
madarakani utawala wa Rais Paul Kagame wa Rwanda.
No comments:
Post a Comment