OMAR Changa, straika aliyekuwa na umbo la mwili lililokuwa
likiendana na nafasi yake hatunaye, na habari kutoka kwa ndugu zake
zinasema alinyongwa na watu wasiojulikana pamoja na kuchomwa na kitu
chenye ncha kali maeneo ya kichwani na ubavuni.
Mchezaji huyo aliyetamba na Yanga alizikwa jana
Jumatatu jioni katika makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Dar es Salaam
huku kifo chake kikiacha maswali mengi ya utata kuliko majibu.
Kwa mujibu wa kaka wa Changa, ambaye alikuwa
mchezaji wa Moro United iliyoshuka daraja, kaka wa marehemu Idd Kambi,
ameliambiaa Mwanaspoti kuwa kwa mujibu wa ripoti ya daktari
aliyokabidhiwa baba wa marehemu, inaonyesha kuwa Omar Changa alichomwa
na kitu chenye ncha kali mgongoni na kilichotokeza mbele ye tumbo huku
pia shingo ikionekana kulegea.
“Mpaka sasa tumemaliza mazishi, lakini bado tuna
huzuni kuhusu hii ripoti tuliyopewa, tunachofanya tunafuatilia ni timu
gani aliichezea mara ya mwisho kwa sababu inaonekana inafichwa, lengo ni
kujua mazingira ya mchezo yalikuwaje.”
Mdogo huyo wa marehemu alisema Omar Changa
alimpigia simu Jumamosi iliyopita, akimtaka kwenda naye kushuhudia
anavyocheza ndondo mchangani maeneo ya Kigamboni nje kidogo ya jiji la
Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Changa alifunga bao moja la ushindi kwa penalti.
Mchumba wake marehemu aliyetambulika kwa jina la
Sarah Mahemba alisema Changa hakurudi kwake tangu alipoondoka Jumamosi
kuelekea Kigamboni katika mchezo huo, jambo ambalo liliwapa shaka
wapangaji wenzake siku ya Jumapili na kuamua kumtafuta kupitia simu yake
ya mkononi lakini haikupatikana ingawa yeye aliijaribu na kuwa inaita
bila kupokelewa mpaka alipopata taarifa za kifo kupitia mdogo wa
mshambuliaji wa Mbeya City, Omari Kijuso.
Mwili wa marehemu ulipatikana katika mtaro, maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment