MECHI za Ligi Kuu Bara zilizohusisha Yanga na Simba na kuchezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wikiendi iliyopita zimeingiza Sh101
milioni.
Yanga ambayo Jumamosi iliyopita iliichapa Ruvu
Shooting mabao 7-0 mechi yake iliingiza Sh68.4 milioni kutokana na
mashabiki 11,972 kuingia uwanjani.
Katika mechi hiyo kila klabu ilipata mgawo wa
Sh15,687,488 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa
kutokana na mapato hayo ni Sh 10.4 milioni. Gharama za tiketi ni Sh3.8
milioni na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilipata Sh 4.8 milioni
wakati uwanja ulipata Sh8.1 milioni.
Gharama za mchezo zilikuwa Sh4.8 milioni wakati
Mfuko wa Maendeleo ya soka (FDF) Sh2.4 milioni. Chama cha Soka Dar es
Salaam (DRFA) na Chama cha Soka Pwani (COREFA) kila kimoja kilipata
Sh945,110.
Simba na JKT Ruvu iliyochezwa juzi Jumapili na
kushuhudiWa na watazamaji 5,850 iliingiza Sh32.7 milioni kwa viingilio
vya Sh5,000, Sh 15,000 na Sh20,000. VAT iliyolipwa ni Sh4.9 milioni.
Kila klabu ilipata mgawo wa Sh7.4 milioni, tiketi
ni Sh2.5 milioni huku gharama za mechi zikiwa Sh 2.2 milioni. Uwanja
ulipata Sh3.7 milioni wakati TPLB walipata Sh2.2 milioni. Mgawo mwingine
ni FDF Sh1.1 milioni na DRFA Sh881,376.
No comments:
Post a Comment