Ukraine imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais
aliyeondolewa madarakani, Victor Yanukovych, Waziri wa mambo ya ndani wa
mpito ametangaza hatua hiyo.
Arsen Avakov amesema katika ukurasa wa Facebook
amesema kesi dhidi yake imefunguliwa dhidi ya Yanukovych na maafisa
wengine kuhusu mauaji ya makubwa ya watu.Wabunge walipiga kura kumuondoa Yanukovych siku ya jumamosi baada ya
maandamano ya miezi kadhaa yaliyojitokeza baada ya kupinga kujiunga na
Umoja wa Ulaya.Machafuko yaliyotokana na maandamano hayo yalisababisha watu kadhaa kupoteza maisha juma lililopita.
Avakov amesema Yanukovych alionekana mjini Balaklava siku ya jumapili, lakini mpaka sasa hajulikani mahali alipo.
No comments:
Post a Comment