STAA wa Bongo Movie, Jacob Stephen maarufu kama JB ameongoza
wasanii wengine tisa kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) katika
sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya chama hicho zilizofanyika jijini
Mbeya jana Jumapili.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape
Nnauye aliwatambulisha wasanii hao ambao baadhi yao walikuwa wamevaa
sare za kijani zinazotumiwa na chama hicho, huku akieleza kuwa
wamejiunga CCM baada ya kutambua ubora wa chama hicho.
Kwenye orodha hiyo, wasanii wa filamu walioungana na JB kuwa wanachama wa CCM ni pamoja na Irene Uwoya, Single
Mtambalike ‘Richie’, Blandina Chagula ‘Johari’,
Tamrina Poshi ‘Amanda’, Haji Adam ‘Baba Haji’, Slim Omari, Salum Haji
‘Mboto’ na Wastara wakati msanii wa muziki ni Banana Zorro.
“Kabla ya kuanza kwa sherehe yetu napenda
kuwatambulisha wasanii wa filamu na muziki ambao wameamua kujiunga na
CCM leo (jana Jumapili), watakabidhiwa kadi zao baadaye na Mwenyekiti wa
chama taifa, Rais Jakaya Kikwete,” alisema Nape.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake JB alisema:
“Naomba mashabiki wetu wote ambao hawana mapenzi na CCM watusamehe sana
kwa uamuzi wetu wa kujiunga na chama hiki. Tumeona ndiyo sehemu nzuri na
tumeamua kujiunga rasmi.”
Naye Wastara alisema: “Tumezaliwa ndani ya CCM, tumekulia CCM na tunaendelea kuishi ndani ya CCM.”
Baadhi ya wasanii wengine waliojitosa kwenye siasa
ni pamoja na Joseph Haule maarufu kama Profesa J, Seleman Msindi
‘Afande Sele’ na Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, ambaye Mbunge wa
Mbeya Mjini kupitia Chadema.
No comments:
Post a Comment