Sunday, 29 September 2013

GETTING RID OF DARK UNDERARMS


LEMON – lemon is a kind of natural cleanser and it also acts as a powerful anti-bacterial and anti-septic. This is why lemon is used in the treatment of various skin related problems including dark underarms. To remove dead skin cells and to lighten skin tone under your arms, take a thick slice of lemon and rub it on the affected area. Wash it off and apply some moisturizer because lemons can cause skin dryness.
I hope this natural home remedies help you out. I know from personal experience that the baking soda works. I’ve slacked off on using it but I’m going to get back into my regimen. Please comment below and share you thoughts, any questions TWEET me @DivaTheBawse
 Soucrce Diva Loveness

MANAGING SMARTPHONE STRESS

so guys simu inaweza kuwa baraka au ni laana it depends on how you use it, kama utaitumia kujifunza vitu vya maana itakuwa engine ya change, kama mkulima akiwa na simu ya mchina na akajua kutumia vizuri akiwa huko Tanga anaweza google kufanya revolution, kupata internet iko pia katika simu ambayo ukiitumia vizuri itakusaidia, je unaitumia kufanya nini? maana pia ni change ya maendeleo,kuna watanzania wangapi wanatumia internet , kumbuka sensa ya mwaka jana ilisema kuna watanzania wangapi? then ukipata asilimia ngapi angalia sehemu ngapi wanatumia internet na ukishapata asilimia hizo angalia watanzania wangapi wanaongea nini au wanatumia social network vipi?
we need freedom of information na hatutaki kuwa controlled on a social network , voice of the People ni social network ,
WHY SOCIAL NETWORK IS POWERFUL ?
To be honest social network is live , unaona emotion za watu tutoe matusi ila social network kupitia simu yako inaweza ku communicate kuhusu ujasiriamali , kufuta umasikini and etc etc , mfano makampuni ya simu siyaelewi mie kama mtanzania nampigia simu mtanzania mwenzangu hapa hapa nakutana na ringtone ya P-SQUARE Badala ya Diamond , why msiondoe ringtone za nje to support our artist na kuwalipa vizuri au mpaka afe ndio muanze Issue zenu za ku support kuuza kazi zake za sanaa kujifanya mnamjali akiwa katika jeneza? doe wake up guys…………………..fanyeni the right thing right about now.
UBAYA WAKE ni kama moto though maana kuna wanaoitumia vibaya , ni kama bunduki inaweza kukuharibu wewe mwenyewe, learned that it reveals a lot about you, inaweza toa focus yako katika mambo muhimu sana learned alot siku hizi za karibuni,
The smarter we become, the more stressed we seem to get. Are you tired of your smartphone running (and ruining) your life?
With your does-it-all smartphone, you’ll never miss a call, text, email, social update, video or anything else that can be beamed into that nifty little device. But is that such a great thing? Your smartphone can increase stress levels — yours, and that of others affected by your always-on habit. mfano mie na twitter lol…you know what am talking about ……… learned from the beast thou to kip it Personal nowdays, how i love this man….. lol. reason i love my Mr.WRONG…My Libra man iks so smarter ……tuishie hapo. no need to drop out the name , ya already know.
Out in public
Just about anywhere in public — on buses, in stores or restaurants, even while waiting for take-off — we’ve all encountered a smartphone user who broadcasts their side of a conversation. While that can sometimes be entertaining, it can get annoying and stressful.
so you decide how to use it , weakness is not the choice.
i am out.

source Diva Loveness

UISLAMU NI UGAIDI AU PROPAGANDA ZA WAHALIFU?


Wengine mnaweza msinielewe, na hamtanielewa kwa sababu tu ya kasumba na taarifa mlizolishwa na watu, na hasa watu wenye mamlaka kwenu, na sana sana hawa wanaweza kuwa viongozi wa dini mnaowaamini.

UGAIDI NA UISLAMU: Wapo watu wanaojaribu kutaka tuamini na kukubaliana nao kwamba eti uislamu ni ugaidi, au waislamu ni magaidi duniani.

MIMI: Naam bado sikubaliani na bado siamini kuwa eti Uislamu ni ugaidi, ninachojua ni kwamba hii ni mbinu chafu ya watu fulani, wenye maslahi fulani wanaotaka kutumia jina la Uislamu kutekeleza uhalifu kwa lengo la kufikia malengo yao.

Na njia pekee ya kufikia malengo yao ni kufanya vitendo vitakavyowajengea watu hofu katika jamii, na pili kuwagawa watu kwa misingi ya udini na siasa ili kutekeleza na kupata maslahi wanayoyataka.

UKWELI KUHUSU HABARI ZA UONGO ZILIZOANDIKWA KWENYE MAGAZETI YA CCM NA SERIKALI KUHUSU WANACHAMA WA CHADEMA WALIOHAMIA CCM MKOANI TANGA WILAYA YA HANDENI

 
 
 
 
 
 
1.SHABANI NGIDO hajawahi kuwa katibu wa wilaya ya handeni wala mwanachama wa chadema kwani katibu wa wilaya ya HANDENI ni LUKASI ELISA SELEMAN kwa hiyo kuhusu katibu wa wilaya chadema kuhamia ccm ni uongo

2.mwenyekiti chadema wilaya ya HANDENI NDIYE KIONGOZI PEKEE ALIYEHAMIA CCM BAADA YA KUMTISHA KUWA WATACHOMA NYUMBA YAKE

3.taarifa za wanachama 300 wa chadema kuhamia ccm ni za uongo badala yake wamehama wanachama 11 na mwenyekiti ni wa 12 tuna daftali la wanachama wa chadema wote wilayani humo.WALIGAWA KADI ZA CHADEMA BANDIA ZILIZOAGIZWA CHINA MWEZI WA 4 MWAKA HUU ZAIDI YA 300 KWA WANACHAMA WA CCM ILI KUUDANGANYA UMMA NA WATU WENYE AKILI NDOGO WAAMINI KUWA CCM IMEVUNA WANACHAMA WAPYA KUTOKA CHADEMA

4.walinunua bendera za chadema kwa gharama ya sh.20,000 hadi 30,000 ilimladi zisipepee sehemu wanazopita kwenye wilaya hiyo

SWALI KWA VIONGOZI WA CCM;udanganyifu huu mnaufanya kwa faida ya nani?MAISHA BORA NA AJILA KWA VJANA NDO HIZI ZA KUWAPA KADI BANDIA ZA CHADEMA?
NI KUKOSA AKILI HEKIMA NA BUSARA KWA VIONGOZI HAWA WA CCM.
Chanzo jamii FORUM.

Megan Young Miss World 2013

Kiama cha wauza unga chaja, faini kuondolewa, kifungo ni cha maisha


Serikali imependekeza marekebisho ya sheria ya kudhibiti dawa za kulevya itakayotoa hukumu ya kifungo cha maisha na kufuta kipengele kwenye sheria ya sasa kinachompa mshtakiwa nafasi ya kulipa faini.
Sheria iliyopo sasa ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya ya mwaka 1995 (Sura ya 95, Ibara ya 16) inasema, endapo mtu atakamatwa kwa kosa la kumiliki, kusafirisha, kuzalisha au kutengeneza mashine ya dawa za kulevya, atahukumiwa kifungo cha maisha jela au kulipa faini ya Sh10 milioni.
Hatua hiyo inakuja wakati idadi ya Watanzania wanaosafirisha, kuzalisha na kutumia dawa hizo ikiongezeka hapa nchini.
Pamoja na mapendekezo hayo, wadau mbalimbali wamesema kufanyika kwa maboresho hayo hakutasaidia kupambana na tatizo lililopo hivi sasa, ikiwa maadili ya wananchi na viongozi yaliyoporomoka hayatarekebishwa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kitila Mkumbo alisema sheria yoyote itakayowekwa haiwezi kuwa ‘mwarobaini’ wa kutibu tatizo la dawa za kulevya hapa nchini kama wanaohusika hawatawajibishwa.
“Hivi sasa zipo sheria, lakini hazitekelezwi. Kuna baadhi ya viongozi wakubwa kabisa wametajwa kujihusisha na dawa za kulevya, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa,” alisema Mkumbo.
Mbunge wa Kawe na Mjumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge, Halima Mdee, alisema Tanzania ina sheria nzuri na bora, lakini changamoto ipo katika utekelezaji wake kwa kuwa rushwa ina mchango mkubwa katika kudhoofisha maendeleo ya taifa.
Mdee alisema ingawa sheria ya rushwa iliyopo hivi sasa ni nzuri, ina kasoro kadhaa zinazohitaji kufanyiwa marekebisho ili kuipa nguvu zaidi.
Alisema baadhi ya viongozi waliopewa dhamana na wananchi wanatuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
“Kama mtandao wa dawa za kulevya tunaousikia upo kuanzia viongozi wakubwa hadi wa chini, unadhani hata ukiwa na sheria nzuri itatekelezwa na nani? alihoji Mdee.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Godfrey Nzowa alisema mapendekezo ya sheria ya dawa za kulevya ni mazuri, lakini yana changamoto nyingi katika utekelezaji wake.

Mtuhumiwa ugaidi Kenya alipitia Arusha


Wakati Serikali ya Kenya imeliomba Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) kumkamata Mwingereza Samantha Lewthwaite (pichani), taarifa zinadai kuwa mwanamke huyo alipitia mpaka wa Namanga, Arusha kwenda Nairobi ambako anahusishwa na tukio la ugaidi.
Lewthwaite, ambaye ni maarufu kwa jina la ‘Mjane mweupe’ inaaminika anashirikiana na kundi la magaidi la Al-Shabab la Somalia.
Kundi hilo ndilo linaaminika lilihusika na mashambulizi kwenye jengo la Westgate jijini Nairobi, wikiendi iliyopita.
Hata hivyo, taarifa ya Interpol ilisema kuwa alikuwa anatakiwa kujibu mashtaka ya kumiliki mabomu na kupanga njama za ugaidi Desemba 2011.
Interpol haikuhusisha maombi hayo ya Serikali ya Kenya na mashambulizi ya Nairobi.
Pia Lewthwaite inasemekana aliingia nchini humo kwa kutumia mpaka wa Tanzania.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Afrika ya Kusini, vinasema mwanamke huyo alitumia pasi ya kusafiri ya nchi hiyo kuingia Kenya kwa kutumia mpaka wa Namanga uliopo mkoani Arusha.
Taarifa hizo zinasema mwanamke huyo alitumia mpaka wa Lunga Lunga na Namanga kati ya Februari na Agosti mwaka 2011 akitumia jina la Webb.

Majina ya Waliopata Mikopo ya Elimu ya Juu 2013/2014 HESLB yatoka. Billion 306 zatengwa...


NOTICE TO SUCCESSFUL LOAN APPLICANTS FOR 2013/2014 ACADEMIC YEAR

The Higher Education Students’ Loans Board is hereby announcing names of successful first time loan applicants for 2013/2014 Academic Year who applied and were eligible for student loans.

The list includes the Institution to which the student is admitted to and the amounts of loans allocated to a particular student in all or part of the loanable items as per Guidelines and Criteria for Issuance of Loans and Grants for 2013/2014 Academic Year.

Loan applicants can access their loan status by keying in their Form Four Index Numbers to view the results. Loan applicants are reminded that the loan money will be sent to their respective institutions where they will be required to sign to acknowledge receipt of the loans, after registration processes.

Issued by:
The Executive Director
Higher Education Students’ Loans Board
P. O. Box 76068
DAR ES SALAAM.

Kujua kama jina lako limo katika waliopata mkopo, tembelea http://olas.heslb.go.tz/

mwanzo Habari Kitaifa Kitaifa Ugaidi Kenya: Kibao chawageukia mawaziri


Nairobi. Shambulizi la kigaidi lililoua watu 67 nchini Kenya wiki iliyopita, limeanza kuchukua sura mpya baada ya kubainika kuwa mawaziri wanne na mkuu wa majeshi walipewa tahadhari kabla kuhusu kutokea kwa tukio hilo.
Taarifa hizo mpya zimekuja wakati ripoti nyingine za uchunguzi zikibainisha kuwa huenda magaidi walioshambulia jengo la Westgate walitoroka kupitia njia ya ardhini inayoanzia kwenye maegesho ya magari chini ya jengo hilo.
Kuhusu mawaziri
Tahadhari hiyo iliyoanza kutolewa Januari mwaka huu, iliwaonya viongozi hao ambao pia ni wanachama wa Baraza la Usalama la Taifa, kuwa Kundi la Al-Shabaab lilikuwa likipanga shambulizi jijini Nairobi.
Kwa mujibu wa ripoti ya kuzuia ugaidi iliyonukuliwa na Gazeti la The Saturday Nation, imewataja Waziri wa Fedha, Julius Rotich, Waziri wa Mambo ya Ndani, Joseph ole Lenku, Waziri wa Ulinzi, Raychelle Omamo, Waziri wa Mambo ya Nje, Amina Mohammed na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Julius Karangi kuwa walikuwa na taarifa za shambulizi hilo.
“Taarifa ilitolewa kwao ikiwatahadharisha kuongezeka kwa vitisho vya ugaidi na mipango ya kuanzishwa kwa mashambulizi mfululizo katika miji ya Nairobi na Mombasa kati ya Septemba 13 na 20, 2013,” inasema ripoti hiyo.
Ripoti hiyo inasema kuwa magaidi walikuwa wakipanga shambulizi linalofanana na lile lililotokea Mumbai, India ambapo walishambulia jengo na kuteka raia.
Pia, taarifa hiyo ilitolewa kwa Kamati ya Ushauri ya Usalama wa Taifa katikati ya Septemba, mwaka huu ambapo taarifa za kiintelijensia zilionyesha kuwa Al-Shabaab wameongeza harakati zao Kenya na kwamba walikuwa wanapanga shambulizi.
Kamati hiyo ambayo ndiyo ngazi ya juu ya usalama nchini Kenya, inajumuisha Rais, Naibu Rais, Waziri wa Ulinzi, Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Majeshi, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na Mkuu wa Jeshi la Polisi.
Viongozi wote waliotajwa kupewa taarifa hawakupatikana, hata ujumbe mfupi wa maandishi waliotumiwa na gazeti hilo kwenye simu zao haukujibiwa.
Shambulizi la wiki iliyopita kwenye jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi, linalomilikiwa wa raia wa Israel, liliua watu 67 na zaidi ya watu 170 kujeruhiwa.

MWALIMU ANAYEDAIWA KULAWITI AKAMATWA

SIKU chache baada ya Gazeti la Majira kuandika habari ya ukatili wa kutisha dhidi ya mwalimu anayedaiwa kuwalawiti wanafunzi wanne mkoani Iringa, mtuhumiwa huyo amekamatwa na yupo katika mikono ya polisi.

Mwalimu huyo anafundisha katika Shule ya Sekondari Wanging'ombe, iliyopo Wilaya Mpya ya Wanging'ombe, mkoani Njombe, Bw. Mwasile Cletus (31).Miongoni mwa wanafunzi waliofanyiwa kitendo hicho mmoja ana miaka10(jina linahifadhiwa),ambaye anasoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Chemchem, mjini humo.
Akizungumza na Majira jana, Kamanda wa Polisi mkoani Iringa,Ramadhan Mungi ,alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Septemba 13 mwaka huu, saa 10 jioni, akiwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Don Bosco, mjini humo jirani na Chuo cha Mkwawa ambako anasoma.
"Mtuhumiwa ni mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza katika Chuo cha Mkwawa, anatuhumiwa kuwalawiti wanafunzi wanne baada ya kuwadanganya kuwa atawapa sh. 200 kila mmoja ili wasitoe siri hiyo kwa wazazi wao," alisema.
Alisema mwanafunzi mmoja wapo kati ya waliolawitiwa, ndiye aliyewaongoza polisi hadi nyumbani kwa mshtakiwa na kuwaonesha chumba walichofanyiwa kitendo hicho .
Aliongezakuwa,upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na jalada lake limetumwa kwa Mwanasheria Mkuu w a Serikali ili kutoa uamuzi kama mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili za kuwalawiti wanafunzi.
Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti,baadhi ya wakazi wa eneo la DonBosco, Kata ya Mkwawa, walisema kama itabainika mtuhumiwa alifanya vitendo hivyo ,atakuwa ameidhalilisha taaluma y a ualimu ambayo inaheshimika duniani kote.
Baadhi ya Wahadhiri wa chuo hicho ambapo hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema kuwa mwanafunzi wao atashindwa kuendelea na masomo chuoni hapo.

BABU WA KIKOMBE LOLIONDO AIBUKA

Mchungaji Ambilikile Mwaisapila (Babu wa Kikombe) wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), amesema Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonesha kuwa Tanzania itakuwa kioo cha Afrika na dunia kwa ujumla.

Alitoa kauli hiyo juzi mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati msafara wa Waziri Mkuu uliposimama nyumbani kwake ili kumsalimia akiwa njiani kurejea mjini Arusha.
Mchungaji Mstaafu Mwaisapila alisema kuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia, lakini hayakutokea Israeli na sasa yatafanyika hapa Samunge.
“Mungu ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee na nitayaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea,” alisema huku akishangiliwa na wananchi.
Alisema katika mafunuo aliyopewa na Mungu ameoneshwa kwamba watu wengi zaidi watafurika kijijini Samunge kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa misaada iliyotoa wakati wa kugawa kikombe ikiwemo mahema, maji na ulinzi.
Waziri Mkuu, Pinda ambaye yuko mkoani Arusha kwa ziara maalum ya kusikiliza matatizo na migogoro ya ardhi yanayowakabili wakazi wa wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale alisema anakubaliana na utabiri wa Mch. Mwaisapila kwani Tanzania imejaliwa gesi nyingi na mafuta mengi ambavyo vitabadili sura ya Taifa hili.
"Mungu ametupa gesi nyingi sana, katika miaka miwili tutakuwa na umeme kila mahali. Tuna makaa ya mawe ambayo ni nishati kubwa na sasa tuna fursa ya kupata nishati ya umeme kutoka ardhini (Geo-thermal) katika Ziwa Natron," alisema.
Alisema Tanzania imekuwa kimbilio la kila mwekezaji na sababu kubwa ni amani na utulivu uliopo nchini. Aliwaeleza wakazi wa Samunge kwamba mapema mwakani mkandarasi wa barabara atakuwa katika eneo lao kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami ambapo awamu ya kwanza itaanzia Wasso hadi Mto wa Mbu kupitia Samunge.

Grace Mbowe, mmewe na mtoto wao wafariki ajalini - Kabuku, Segera - Tanga


Kuna ajali mbaya imetokea asubuhi hii eneo la Segera ambapo gari aina ya GX100 limepinduka na kuuwa watu watatu ambao walikuwa abiria wa gari hilo.

Card ya gari inasemekana ina jina la mmiliki aitwae Grace aikaeli Mbowe. Grace Mbowe mwanamama aliyedaiwa  kuhamia CCM wilayani Hai ni dada wa mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.

Friday, 27 September 2013

Miezi 6 jela kwa wimbo wa matusi Tunisia


Msanii wa kizazi kipya nchini Tunisia, Ahmed Ben Ahmed, anayejulikana kwa jina la kiusanii, Klay BBJ, amehukumiwa jela kwa miezi sita kwa kuwatusi maafisa wakuu kupitia kwa muziki wake.
Mahakama ilitupilia mbali kesi yake ya rufaa baada ya yeye na mwanamuziki mwenzake kupatikana na hatia mwezi jana ya kuwatusi maafisa wakuu katika tamasha la muziki eneo la Hammamet.
Wawili hao awali walihukumiwa bila ya wao kuwepo mahakamani kutumikia kifungo cha miezi 21 lakini hukumu hiyo iliondolewa.
Weld El 15, aliyepatikana na kosa kwa kuimba wimbo wake huo, kuwa 'Ploisi ni Mbwa', hakukata rufaa na sasa yuko mbioni.
Hata hivyo Kaly BBJ lisema kuwa wimbo wao ulikuwa unaelezea hali ilivyo nchini Tunisia na kuhusu serikali.
Muungano wa vyama unaoongozwa na chama cha wanasiasa waisilamu wenye msimamo wa kadri, Ennahda, uliingia mamlakani baada ya mapinduzi ya kiraia yaliyomwondoa mamlakani aliyekuwa rais Zine el-Abidine Ben Ali mwezi Januari mwaka 2011 na uchaguzi kufanyika baadaye mwaka huo.
Klay anasemekana kuambia mahakama kuwa wimbo wao unakosoa hali ya sasa serikalini na kote nchini Tunisia tu.
Alisema yeye ni mmoja wa wanamuziki wanaokosoa sana serikali na ndio maana wamekuwa wakimsaka sana.
Lakini majaji walikataa rufaa aliyowasilisa na kusema hukumu yake ya miezi sita gerezani inastahili kuanza mara moja.
Wakili wake alisema kuwa watawasilisha rufaa nyingine kupinga hukumu dhidi yake.

UN yajadili azimio kuhusu Syria


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linajadili rasimu ya azimio kuhusu silaha za kemikali za Syria baada ya Marekani na Urusi kukubali mapendekezo ya azimio hilo.
Wanachama kumi na tano wa baraza hilo huenda wakapigia kura azimio hilo baadaye leo, hii ni kwa mujibu wa wanadiplomasia katika umoja wa Mataifa.
Makubaliano hayo yanamaliza mvutano wa miaka miwili na nusu katika Umoja wa mataifa kuhusu Syria.
Inaonekana kama hatua muhimu katika mwafaka unaosakwa sana kwa ushirikiano wa Marekani na Urusi ambapo Syria itafichua zana zake za kemikali na kuziharibu ifikapo mwaka 2014
Urusi na China mara tatu zimekuwa zikizuia maazimio ya nchi za magharibi katika baraza la usalama dhidi ya Rais wa Syria, Bashar al-Assad.
Baraza hilo lilijadili azimio hilo Alhamisi Jioni katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Kabla ya mkutano huo Marekani na Urusi zilitofautiana kuhusu maandiko na mapendekezo ya azimio hilo.
Marekani kwa ushirikiano na Ufaransa na Uingereza, zilikuwa zimependekeza kuchukau hatau za kijeshi dhidi ya Syria.
Urusi nayo ilipinga azimio hilo kwa sababu ya tisho la kuvamia Syria kijeshi.
Mataifa hayo ni wanachama wenye uwezo wa kupiga kura ya turufu dhidi ya pendekezo lolote katika baraza hilo.

Polisi wamchunguza Agathon Rwasa

Viongozi wa mashtaka nchini Burundi wametangaza kuwa wameanzisha uchunguzi dhidi ya aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini humo Agathon Rwasa kutokana na tutuma za kuhusika na mauaji ya wakimbizi miaka tisa iliyopita.
Wakimbizi nchini Burundi walikuwa wamewasilisha malalamishi dhidi ya bwana Rwasa ambaye wanadai kuwa aliamuru mauaji ya watu 160 wenye asili ya Kitutsi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya katika kambi ya wakimbizi ya Gatumba Magharibi mwa mji mkuu wa Burundi, Bujumbura mwaka 2004.
Bwana Rwasa aliwahi kuwa kiongozi wa kundi la waasi la FNL ambalo sasa limegeuka na kuwa chama cha kisiasa.
Alitoroka nchini Burundi mwaka 2010 baada ya uchaguzi uliozua utata ambapo rais wa sasa President Pierre
Nkurunziza alitangazwa mshindi.
Amejitokeza tena mwezi uliopita na kutangaza kuwa atarejea katika siasa za burundi.
Mwandishi wetu wa Bujumbura Kazungu Lozy amezunguza na bwana Agathon Rwasa kuhusiana na hatua hiyo ya upande wa mashtaka.

Msako dhidi ya wahamiaji haramu Tanzania

Zaidi ya watu sabini wanaodai kuwa ni raia wa Tanzania wamegoma kuendelea na safari kuingia nchini Rwanda baada ya vyombo vya dola nchini Tanzania kuwafikisha kwenye mpaka wa Rusumo kati ya mataifa mawili.
Awamu ya kuwaondosha kwa nguvu wamamiaji haramu kutoka Tanzania kwa agizo la rais Jakaya Kikwete imeanza mwishoni mwa juma,baada takriban wanyarwanda elfu saba kurejea hapo awali kwa hiari yao japo baadhi walidai kuyakimbia maskani yao kutokana navitisho kadha wa kadha dhidi yao.
Mwandishi wa BBC John alikwenda katika mpaka wa Rusumo kujionea hali

Walinipiga risasi lakini nikaponea











Watu 62 wamefariki katika shambulii la kigaidi lililofanywa na magaidi wa Al Shabaab katika jengo la Westgate na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa. Magaidi hao walivamia jengop la Westgate siku ya Jumamosi mchana na kuwafyatulia risasi kiholea watu waliokuwa ndani ya jengo hilo.
Vikosi vya usalama vimeweza kudhibiti jengo hilo na kuwaua magaidi tisa. Hata hivyo baadhgi ya watu waliweza kunusurika kifo kwa kukimbilia usalama wao na wengine labda kwa kutokuwa tu katika ghorofa ambako wanamgambo hao walifanya mashambulizi.
Mmoja wa wale walionusurika ni Salpat Singh

Kenya yamsaka Samantha Lewthwaite

Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu wanaosakwa sana duniani.
Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.
Bi Lewthwaite, mwenye umri wa miaka 29, ni mjane wa mlipuaji aliyefanya shambulizi la kujitoa mhanga mjini London Uingereza mwezi Julai mwaka 2005
Anajulikana kama "white widow", na amehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini Somalia.
Polisi wa Interpol hata hivyo hawakuhusisha hatua ya kumsaka Samantha na shambulizi la kigaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi lililowaua watu 67.
Hata hivyo, hatua hii ya kumsaka Bi Lewthwaite inakuja punde baada ya shambulizi hili la kigaidi nchini Kenya.
Al-Shabab ilikiri kufanya mashambulizi hayo yaliyotokana na kutekwa kwa jengo la Westgate na kisha kutekwa kwa raia wa kawaida waliokuwa ndani ya jengo hilo kwa siku nne.
Kwa mujibu wa polisi wa Interpol, mwanamke huyo anasakwa na serikali ya Kenya kwa kumiliki mabomu na kupanga njama ya kufanya mashambulizi kuanzia Disemba mwaka 2011.
Ikiwa mwanamke huyo atakamatwa katika nchi mwanachama wa Interpol, atazuiliwa na kusibiri kupelekwa katika nchi anayotakikana kwa kesi kufunguliwa dhidi yake.
Bi Lewthwaite anajulikana kwa jina bandia la, "Natalie Webb" –na alikuwa anasakwa kwa madai ya kumiliki hati bandia ya usafiri nchini Afrika Kusini.
Ni mjane wa Germaine Lindsay, mmoja wa washambuliaji wanne waliohusika na shambulizi la kigaidi mjini London ambapo watu 52 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa.