UISLAMU NI UGAIDI AU PROPAGANDA ZA WAHALIFU?
Wengine
mnaweza msinielewe, na hamtanielewa kwa sababu tu ya kasumba na taarifa
mlizolishwa na watu, na hasa watu wenye mamlaka kwenu, na sana sana
hawa wanaweza kuwa viongozi wa dini mnaowaamini.
UGAIDI NA
UISLAMU: Wapo watu wanaojaribu kutaka tuamini na kukubaliana nao kwamba
eti uislamu ni ugaidi, au waislamu ni magaidi duniani.
MIMI: Naam bado sikubaliani na bado siamini kuwa eti
Uislamu ni ugaidi, ninachojua ni kwamba hii ni mbinu chafu ya watu
fulani, wenye maslahi fulani wanaotaka kutumia jina la Uislamu
kutekeleza uhalifu kwa lengo la kufikia malengo yao.
Na njia
pekee ya kufikia malengo yao ni kufanya vitendo vitakavyowajengea watu
hofu katika jamii, na pili kuwagawa watu kwa misingi ya udini na siasa
ili kutekeleza na kupata maslahi wanayoyataka.
No comments:
Post a Comment