SIKU chache baada ya Gazeti la Majira kuandika
habari ya ukatili wa kutisha dhidi ya mwalimu anayedaiwa kuwalawiti
wanafunzi wanne mkoani Iringa, mtuhumiwa huyo amekamatwa na yupo katika
mikono ya polisi.
Mwalimu
huyo anafundisha katika Shule ya Sekondari Wanging'ombe, iliyopo Wilaya
Mpya ya Wanging'ombe, mkoani Njombe, Bw. Mwasile Cletus (31).Miongoni
mwa wanafunzi waliofanyiwa kitendo hicho mmoja ana miaka10(jina
linahifadhiwa),ambaye anasoma darasa la nne katika Shule ya Msingi
Chemchem, mjini humo.
Akizungumza na Majira jana,
Kamanda wa Polisi mkoani Iringa,Ramadhan Mungi ,alisema mtuhumiwa huyo
alikamatwa Septemba 13 mwaka huu, saa 10 jioni, akiwa kwenye nyumba
aliyokuwa akiishi eneo la Don Bosco, mjini humo jirani na Chuo cha
Mkwawa ambako anasoma.
"Mtuhumiwa
ni mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza katika Chuo cha Mkwawa, anatuhumiwa
kuwalawiti wanafunzi wanne baada ya kuwadanganya kuwa atawapa sh. 200
kila mmoja ili wasitoe siri hiyo kwa wazazi wao," alisema.
Alisema
mwanafunzi mmoja wapo kati ya waliolawitiwa, ndiye aliyewaongoza polisi
hadi nyumbani kwa mshtakiwa na kuwaonesha chumba walichofanyiwa kitendo
hicho .
Aliongezakuwa,upelelezi
wa kesi hiyo umekamilika na jalada lake limetumwa kwa Mwanasheria Mkuu w
a Serikali ili kutoa uamuzi kama mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani
kujibu tuhuma zinazomkabili za kuwalawiti wanafunzi.
Wakizungumza na Majira kwa
nyakati tofauti,baadhi ya wakazi wa eneo la DonBosco, Kata ya Mkwawa,
walisema kama itabainika mtuhumiwa alifanya vitendo hivyo ,atakuwa
ameidhalilisha taaluma y a ualimu ambayo inaheshimika duniani kote.
Baadhi
ya Wahadhiri wa chuo hicho ambapo hawakutaka majina yao yaandikwe
gazetini, walisema kuwa mwanafunzi wao atashindwa kuendelea na masomo
chuoni hapo.
No comments:
Post a Comment