Zaidi ya watu sabini wanaodai
kuwa ni raia wa Tanzania wamegoma kuendelea na safari kuingia nchini
Rwanda baada ya vyombo vya dola nchini Tanzania kuwafikisha kwenye mpaka
wa Rusumo kati ya mataifa mawili.
Awamu ya kuwaondosha kwa nguvu wamamiaji haramu
kutoka Tanzania kwa agizo la rais Jakaya Kikwete imeanza mwishoni mwa
juma,baada takriban wanyarwanda elfu saba kurejea hapo awali kwa hiari
yao japo baadhi walidai kuyakimbia maskani yao kutokana navitisho kadha
wa kadha dhidi yao.Mwandishi wa BBC John alikwenda katika mpaka wa Rusumo kujionea hali
No comments:
Post a Comment