KOCHA wa Simba, Zdravko Logarusic amesema aliamua kumtoa straika
Betram Mwombeki dakika 20 baada ya kumuingiza dhidi ya Rhino Rangers
ili kumsitiri kwa aibu ambayo angeipata kutoka kwa mashabiki.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana
Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa
bao 1-0, Logarusic alimuingiza Mwombeki dakika ya 65 kuchukua nafasi ya
Amissi Tambwe.
Dakika chache baada ya kuingia uwanjani, Mwombeki
alipoteza pasi tatu ndani ya dakika nane hali iliyomfanya Logarusic
ampigie kelele za kuelekeza kila anapokosea.
Mara kadhaa Mwombeki alipokuwa akikosea alionekana
kujutia kosa lake kwa kujaribu kukaba ili apokonye mpira aliopoteza,
lakini Logarusic alikuwa akishika kichwa kuonyesha kutopendezwa na
makosa hayo. Uvumilivu ulimshinda kocha huyo kwani dakika 85 alimtoa
Mwombeki na kumuingiza Henry Joseph. Wakati anatoka straika huyo
alisalimiana na Logarusic ikiwa ni ishara ya kutokuwepo kwa tatizo baina
yao.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Logarusic alisema
alilazimika kumtoa Mwombeki kutokana na kushindwa kutimiza alichotumwa
uwanjani akitokea benchi pia kumsitiri kwa aibu ya kuzomewa na
mashabiki.
“(Mwombeki) alikuwepo benchi kuona makosa ya
wenzake, lakini alipoingia kila mtu ameona alichokuwa anafanya,
mashabiki wakaanza kumpigia kelele ndipo nikaona nimsitiri kwa kumtoa
maana angebaki angepata aibu zaidi,”Mwanasipoti
No comments:
Post a Comment