Kati ya vigogo aliokuwa akipambana nao ndani ya
CCM ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa
Mwangunga na aliyekuwa mkuu wa wilaya kadhaa, Hawa Ng’umbi ambaye ndiye
alishinda.
Hata hivyo, Ng’umbi alibwagwa na John Mnyika wa
Chadema. Lilikuwa ni pigo kubwa mno kwa CCM na hasa kwa Nape ambaye
alishajipambanua kama mpenda mageuzi ndani ya chama.
Alishajiwekea rekodi ya kufichua ufisadi ndani ya chama hicho hasa ule wa ujenzi jengo la Umoja wa Vijana pale Lumumba.
Hapo ndipo zikaanza kusikika tetesi kuwa Nape
alitaka kuhamia Chadema, mara wengine wakimhusisha na chama kipya wakati
huom cha CCJ (sasa CCK) kilichokuwa kikidaiwa kuanzishwa na baadhi ya
vigogo wa CCM wasioridhishwa na mwenendo wa chama hicho tawala.
Lakini CCM nao walionekana kuushtukia mchezo huo.
Siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 mara Nape akafutwa
machozi na Rais Jakaya Kikwete alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya
Masasi. Ilikuwa kama gia ya kumshikilia asije kukimbilia vyama vingine.
Aliishikilia nafasi hiyo hadi mapema Machi, 2011
ambapo CCM ilifanya mabadiliko ya sekretarieti. Hapo Nape akapewa nafasi
ya Katibu wa Itikadi na uenezi anayoishika hadi sasa, huku nafasi ya
Katibu Mkuu akipewa Wilson Mukama.
Mabadiliko hayo yalikwenda sanjari na mkakati wa
kujivua gamba. Hapo mhemko tena wa Nape na viongozi wenzake kukisafisha
chama na ufisadi ukaanza pale waliposisitiza kuwa lazima wale
wanaochafua sura ya chama wawajibishwe.
Sote ni mashahidi, hadi leo hakuna aliyevuliwa gamba. Chama kinaendelea kusonga mbele na magamba yake.
Juzi juzi tena baada ya sekretarieti ya chama
kubadilishwa na Abdulrahman Kinana kuwa Katibu Mkuu, Nape akabebeshwa
mzigo la kutaja mawaziri mizigo. Wakawashikia kidedea hadi Kamati Kuu ya
CCM ili wahojiwe. Wamehojiwa lakini baadaye wamerejeshwa barazani.
Mara Nape kaibuka tena mbele ya waandishi wa
habari akisema eti CCM hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya mawaziri
na watendaji wengine watakaoshindwa kurekebisha upungufu unaopigiwa
kelele.
Itachukua hatua gani, wakati Mwenyekiti wa chama
Rais Kikwete amesharidhika na mizigo yake? Ni kama vile Nape anatamani
yeye ndiye angekuwa rais ili awafurumushe mawaziri hao, lakini basi
hawezi….!
Hiyo ndiyo CCM. Utamaduni wa kuwajibishana na kufukuzana haupo.
Mwenzako akifanya kosa unamezea. Kama Nape anaona kasi yake haiendani na
CCM, bora atafute chama kingine ahamie.
Vinginevyo atakuwa anapiga kelele za bure huku wenzake wakiendelea kuchukua vyao mape
Mwananchi
No comments:
Post a Comment