Rais wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell, amejiuzulu
kufuatia madai ya utumizi mbaya wa fedha wakati klabu hiyo ilipomsajili
nyota wa Brazil, Neymar mwaka uliopita.
Bwana Rosell, amesema madai yanadhamiria
kumharibia sifa na kuwa haya sio ya kweli lakini amehisi hadhi ya
heshima ya klabu hiyo itahujumiwa ikiwa ataendelea kuhudumu kama rais wa
klabu hiyo.Mapema wiki hii, gazeto moja nchini Uhispania ilinadi kuwa, klabu hiyo ilitumia Uro milioni arubaini zaidi kuliko ilivyotangazwa kumsajili mchezaji huyo kutoka Brazil.
Ripoti zinasema kuwa babake Neymar na mawakala wengine waliohusika na mkataba huo walilipwa kiasi fulani cha pesa ambacho hakikutangazwa.
No comments:
Post a Comment