BEKI Shomari Kapombe, yupo mjini Morogoro akifikiria jinsi ya
kurudi katika klabu yake ya AS Cannes ya Ufaransa, lakini uchunguzi
umeonyesha kwamba Simba, imebariki nyota huyo kutua Yanga au Azam FC
endapo zitafikia makubaliano na Cannes.
Uchunguzi uliofanywa na Mwanaspoti, umebaini
kwamba, kwa mujibu wa mkataba ambao Simba ilisaini na Cannes, wakati
akiuzwa kupelekwa kwa Wafaransa hao ni kwamba beki huyo aliuzwa kwa
klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Katika mkataba huo, ambao Mwanaspoti imepata
sehemu ya nakala yake, uliosainiwa na Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden
Rage na Rais wa Cannes, Simba imemruhusu Kapombe kuuzwa kwa klabu
yoyote duniani endapo itafikia dau litakalohitajika, hatua ambayo inatoa
fursa kwa klabu za Yanga, Azam FC Ashanti United na hata Galatasaray ya
Uturuki kama zikimuhitaji.
Sehemu hiyo ya mkataba huo, inaonyesha kwamba
endapo Kapombe atauzwa katika klabu yoyote duniani, Simba itavuna
asilimia 40 ya mauzo hayo sambamba na Cannes ambao nao watapata mgawo
kama huo, huku wakala wake Denis Kadito anayeishi Uholanzi akipata
asilimia 20.
Wakala wa beki huyo, Kadito amezitaka klabu
zinazomtaka mchezaji huyo kufuata utaratibu kwa kuzungumza na Cannes au
yeye lakini kinyume na hapo zinajisumbua.
Mwanasipoti
Mwanasipoti
No comments:
Post a Comment