KIPA Ally Mustapha ‘Barthez’ alimkimbia Juma Kaseja na kutimkia
Yanga kutokana na kukosa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza cha Simba
na sasa Kaseja amerejea Yanga kwa mara nyingine.
Kaseja ambaye aliachwa na Simba baada ya kumaliza mkataba wake amesaini Yanga kwa kitita cha Sh40 milioni.
Barthez alikuwa kipa namba mbili wa Simba wakati ikinolewa na kocha aliyetupiwa virago, Mserbia Milovan Cirkovic.
Kaseja alisimama lango la Simba kwenye mechi zote
za ligi kwa misimu miwili mfululizo pasipo kumwachia Barthez kudaka
angalau mechi moja zikiwemo za kirafiki.
Benchi lilimkimbizia Barthez Yanga ambako sasa Kaseja amemfuata huko huko.
Mbali na Barthez kipa mwingine aliyekimbia benchi
la Simba ni Deo Munishi ‘Dida’ ambaye kwenye mechi nne za mwisho kwenye
ligi msimu huu alianza kuonyesha kiwango kizuri huku akiwa hajaruhusu
bao hata moja kutinga kwenye nyavu zake lakini kuingia kwa Kaseja Yanga
kunamuweka pabaya kupata namba.
Yanga kwa mara ya kwanza inasajili makipa watatu ambao wote waliwahi kuchezea Simba na tena walikuwa wote.
Dida na Barthez wamegoma kuzungumza lolote kuhusu
usajili wa Kaseja ingawa habari za uhakika zinadai kwamba hawakutarajia
hali hiyo kutokea.
Wakati anasajiliwa Barthez mashabiki wa Yanga
walikuwa wakipaza sauti kwenye mechi za Simba msimu 2010/11 wakimtaka
Barthez kumkimbia Juma Kaseja na kujiunga na Yanga ambayo ilikuwa na
makipa Said Mohammed na Mghana Yaw Berko ambaye alikuwa akisumbuliwa na
maumivu ya bega mara kwa mara.
Barthez alijiunga Yanga mwaka jana na kuipa
ubingwa wa ligi ukiwa msimu wake wa kwanza ingawa msimu wake wa pili
umekuwa mbaya baada ya kupoteza namba kwenye kikosi cha kwanza tangu
Yanga ilipotoka sare ya mabao 3-3, Oktoba 20.
Habari za ndani zinadai awali mwaka jana benchi la
ufundi la Yanga lilimpa Barthez nafasi ya kuchagua kipa atakayefanya
naye kazi lakini hakumtaka Kaseja, alimchagua Dida na ndiye
aliyesajiliwa.
Mwanaspoti
Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment