MTANZANIA ambaye jina lake limehifadhiwa aliyekamatwa Uwanja wa Ndege
wa Mumbai, Jumatau ya wiki hii nchini India akiwa na madawa ya kulevya
amefariki dunia.
Alilalamika kuwa anaumwa tumbo baada ya kukimbizwa na kukamatwa na wanausalama wakati akijaribu kutoroka na alifariki wakati anakimbizwa hospitali. Alikutwa na pipi 120 za cocaine tumboni mwake kila moja ikiwa na uzito wa gramu kati ya 12 na 15.
Marehemu alikuwa na mwenzake ambaye amekutwa na pipi 60 tumboni
mwake. Inaonekana watuhumiwa hawa hawakuwa na uzoefu wa dawa za kulevya
"Tofauti na wenzao ambao hukataa chakula na maji, Watanzania hawa
walipopewa maji na chakula walikubali kirahisi jambo ambalo ni hatari
kwa wabebaji wa dawa hizo maana chakula husukuma dawa hizo chini na
kusababisha zipasuke.Alilalamika kuwa anaumwa tumbo baada ya kukimbizwa na kukamatwa na wanausalama wakati akijaribu kutoroka na alifariki wakati anakimbizwa hospitali. Alikutwa na pipi 120 za cocaine tumboni mwake kila moja ikiwa na uzito wa gramu kati ya 12 na 15.
Watanzania hao ambao majina yao bado yamehifadhiwa walikamatwa baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Mumbai majira ya saa 10 alfajiri Jumatatu ya wiki hii.
"Baada ya kuwashtukia kuwa wana dawa za kulevya, Watanzania hao walikana kuwa na mizigo hiyo, ndipo tukawapekua mizigo yao lakini hawakuwa na kitu." Alisema ofisa mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Mumbai.
"Mmoja wa watuhumiwa alisema amekuja India kwa matibabu ya bega. Japo alionyesha nakala ya barua pepe ya Hospitali ya Mumbai ambayo ilikuwa ikimuonyesha kuwa ni mgonjwa anayesumbuliwa na tumbo." Alisema ofisa huyo.
Wanausalama wa uwanja wa ndege waliamua kuwapeleka mahakamani majira ya saa 11 jioni kupata kibali cha kuwapiga X-rays.
Walipofika mahakamani marehemu alijaribu kutoroka na kukamatwa na maofisa hao. Baada ya dakika chache alianza kulalamika kuwa ana maumivu umboni na kulala chini. Alichukuliwa na gari la kubebea wagonjwa 'ambulance' kupelekwa hospitali lakini alipoteza maisha njiani. "Mapovu meupe yalikuwa yakimtoka mdomoni marehemu alipokuwa katika ambulance." Walisema maofisa hao.
Baada ya mwenzake kufariki, mtuhumiwa mwingine alikiri kubeba dawa za kulevya na kutolewa pipi 60 Jumanne usiku.
"Baada ya kutoa pipi zote, tutafanya uchunguzi wa madawa haya kujua ni kiasi gani na thamani yake" walisema wa Uwanja wa Ndege wa Mumbai.
No comments:
Post a Comment