amempongeza
kiungo wake chipukizi, Hassan Dilunga kusaini Yanga SC, lakini
amemuambia asipokuwa makini atapotea ndani ya muda mfupi tu kwenye
ramani ya soka.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY usiku huu, Mkwasa amesema kwamba Dilunga ni mchezaji mzuri na amekuwa tegemeo lake Ruvu Shooting, hivyo kwenda kwake Yanga ni pigo kwa timu yake.“Ni mchezaji ambaye tumekuwa naye tangu akiwa mdogo, tumemlea vizuri hapa hadi amekuwa tegemeo la timu. Kwa kweli nafurahia mafanikio yake, kwanza kuitwa Stars (timu ya taifa) na pia kusajiliwa Yanga.
Yanga ni timu kubwa, wazi atapata maslahi mazuri, lakini anatakiwa akazane katika mazoezi ili awe fiti zaidi na kuweza kugombea namba pale Yanga, kwa sababu kuna wachezaji wazuri sana wa nafasi yake,”alisema.
Mkwasa alisema iwapo Dilunga hatajibidiisha katika mazoezi na kujikuta anakosa namba katika kikosi cha kwanza Yanga, maana yake atapoteza nafasi T“Kwa kweli Dilunga asipokuwa makini atapotea ndani ya muda mfupi. Bado kijana mdogo na kusajiliwa Yanga ni nafasi nzuri kwake kukuza kipaji chake, ila lazima ajitambue na atambue changamoto zinazomkabili,”alisema.
Dilunga anaingia kwenye orodha ya viungo kibao na wote mafundi waliopo Yanga SC, akina Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo ambao pia ni wapinzani wake wa namba Taifa Stars, Nizar Khalfan, Haruna Niyonzima, Salum Telela na Hamisi Thabit.
Kiungo huyo amesaini jana usiku Mkataba wa miaka mitatu na Yanga, ingawa uongozi wa Ruvu Shooting umekaririwa leo ukisema, bado ana Mkataba pia na timu hiyo ya jeshi.aifa Stars na mwisho wa siku klabu hiyo pia itamtoa kwa mkopo na huo ndiyo ukawa mwisho

No comments:
Post a Comment