STEWART Hall amethibitisha kuwa alivunja mkataba na Azam FC
mwezi uliopita lakini wakakubaliana iwe siri kati yake na kigogo wa timu
hiyo Abubakar Bakhresa.
Hata hivyo kocha huyo ameweka wazi kuwa alisaini mkataba muda huohuo na timu nyingine ya Bongo ingawa hakuiweka wazi.
“Tulizungumza na Abubakar, alinikubalia na ikabaki
siri kati yangu na yeye, niliendelea na timu ili kumpa nafasi atafute
kocha mwingine. Nisingeweza kuondoka hivyo, malengo yalikuwa kumaliza
mzunguko wa kwanza kileleni ingawa tumekuwa wa pili,” alisema Hall.
“Nimekaa muda mrefu Azam, nimefanya mengi mazuri
lakini si kila kiongozi aliridhika, hata wakati mwingine ningeshinda
michezo mingi lakini kuna viongozi ambao hawakunitaka. Kibaya zaidi
viongozi hao hawakupenda ukaribu wangu na wachezaji, niliona na kushauri
lakini nilipigwa vita,” alisema.
“Mpira wa Tanzania umejaa siasa, wachezaji wote ni
bora lakini pongezi zangu za heshima kwa Aggrey Moris na Waziri Salum
kwa kuwa wachezaji wangu bora, ingawa pia Kipre Tchetche alifanya kazi
nzuri,” alisema.
Kuhusu wapi aliposaini mkataba kama mkurugenzi wa
ufundi kocha huyo alisema: “Siwezi kusema lolote, mfano nikisema
ninaenda Simba, sitokuwa nimelifanyia haki benchi la ufundi au kocha
aliyepo Simba sasa.”
No comments:
Post a Comment