Akizungumzia elimu kwa watoto na wajukuu wake, anasema hiyo siyo
kipaumbele kwake, huku akisisitiza kuwa kuna uhaba wa shule katika
kijiji hicho.
“Watoto hawa hawasomi, tatizo huku hakuna shule,
hata wenyeji wa huku hawasomi kazi ni kukata miti tu. Hata hivyo kuna
watoto wangu wako Tabora ndiyo wamesoma, lakini sijui wamefikia darasa
la ngapi,” anasema.
Ndoa za utotoni
Mbali na mzee Singu, yupo mjukuu wake, Jiraa
Lukanda Lukata anayekadiriwa kuwa na miaka 30 anayeonekana kufuata nyayo
za babu yake.
Jiraa ameoa wake watatu na anaishi na babu yake
kwenye boma hilo. Kwa mke wa kwanza, Gindu Shija mwenye umri wa miaka 21
ana watoto wanne huku mke wa pili, Lawi Kulwa (miaka 21) na Holo Shija
(miaka 15) walioolewa miaka miwili iliyopita bado hawajapata watoto.
Hata hivyo, Jiraa anakanusha kufuata nyayo za babu yake:
“Siyo kwamba nafuata nyayo za babu, mimi naishia hawa wake watatu tu wanatosha,” anasema Jiraa.
Akieleza taratibu za kupata wake hao, Jiraa anasema wazee hasa babu yake wamehusika kumtafutia.
“Kwa taratibu zetu za Kisukuma, wazee huchunguza
wanawake wenye tabia nzuri kutoka kwenye koo nyingine. Hawa wake zangu
babu yangu alinioza baada ya kuridhishwa na tabia zao,” anasema na
kuongeza:
“Mke wa kwanza nilimwolea katika kijiji cha Muhoro hapa hapa Rufiji.
Akizungumzia ufahamu wake kuhusu sheria za ndoa
anasema licha ya kutokuwa na elimu yoyote anazifahamu sheria
zinazokataza ndoa za utotoni.
“Mimi sina elimu yoyote wala wake zangu hawana
elimu, lakini naelewa baadhi ya sheria za ndoa. Najua sijafanya kosa
kosa lolote kuoa wake wenye umri huu,” anasema.
Chanzo Mwananchi
Chanzo Mwananchi
No comments:
Post a Comment