Monday, 11 November 2013

Wakamatwa kwa biashara haramu ya ngono


Polisi nchini Uhispania, wamewakamata watu 25 wanaoshukiwa kuhusuka na sakata ya biashara ya ngono.
Washukiwa hao wanadaiwa kujihusisha na biashara ya kuwaleta wanawake kutoka Nigeria kufanya kazi kama makahaba nchini humo.Wanawake hao waliodanganywa kwa mara ya kwanza kuwa watapata kazi nzuri barani Ulaya, mwanzo walipelekwa Mexico au Brazil wakisafiri kwa kutumia hati bandia za usafiri.

Kisha kutoka hapo, walisafirishwa hadi mjini Paris na kisha kuingizwa kimagendo nchini Uhispania kufanya kazi kama makahaba.
Polisi walisema kuwa wanawake 5 waliokuwa waathiriwa wa sakata hiyo waliachiliwa wakati wa msako.
Polisi walimkuta mmoja wa wanaume hao akimsaidia mwanamke mmoja kuavya kimba , kwa mujibu wa mwandishi wa BBC mjini Madrid,Tom Burridge.
Polisi waliwakamata watu kadhaa katika sehemu mbali mbali nchini Uhispania ikiwemo, mjini Madrid, Toledo, Cantabria na Palma de Mallorca.
Zaidi ya magari 100 yaliyokuwa na bidhaa za kifahari yalikamatwa.
Polisi walisema kuwa genge hilo lilitumia magari hayo kufanyia biashara haramu na kisha kupeleka faida nyumbani, Nigeria
Aidha polisi wanasema genge hilo liliundwa miaka 20 iliyopita katika vyo vikuu vya Nigeria, wanaojulikana kwa kuwatumia watu barua za kuomba pesa.
Watu 8 kati ya 25 waliokamatwa, walikuwa wanaishi nchini Uhispania kinyume na sheria.

No comments:

Post a Comment