Kwa kifupi unaweza kusema huu si mwaka wa Leonel Messi.
Alizoeleka kwa uwezo wake mkubwa wa kufunga na kunyanyasa mabeki, lakini sasa nyota huyo anaandamwa na majeraha.
Uso wake unazungumza yote, nyota huyo anasumbuliwa
na tatizo la misuli ambayo sasa yatamfanya kukosa mechi zote
zilizobakia kwa mwaka huu.
Matatizo yote yalianza Aprili 2 kwenye Uwanja wa
Parc des Princes walipocheza dhidi ya PSG. Hapo ndipo alipoanza
kusumbuliwa na tatizo la misuli.
Alimaliza msimu katika kiwango ambacho si chake na
alitegemea baada ya mapumziko wa majira ya joto mambo yangebadilika kwa
kuwa Messi hakukuwa na mashindano ya Olimpiki, Kombe la Dunia wala Copa
Amerika.
Hata hivyo, Messi kwa mara nyingine alionekana
hayuko fiti wakati wa ziara ya Barca barani Asia. Baada ya mechi ya
kwanza ya Spanish Super Cup dhidi ya Atletico, ugonjwa wa misuri
ukamrudia tena.
Mwishoni mwa Septemba, mjini Almeria ilitolewa
taarifa kwamba Messi bado hayuko fiti. Jumapili iliyopita Messi ameumia
tena kwa mara ya nne na sasa mjini Seville na atakaa nje kwa miezi
miwili.
Labda apone kwa haraka kuliko inavyotegemewa, la sivyo nyota huyo wa Argentina ataufunga mwaka huu akiwa na mabao 42 tu.
No comments:
Post a Comment