Kwa kitaalamu, ugonjwa wa akili ya ngono wa kupenda kuacha mwili wazi unaitwa ‘exhibitionism’ ambapo mtu huweza kuamua kuacha maziwa, mapaja au kwa wanaume kuvaa suruali inayoelekea kuanguka kutoka maungoni,” Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili na mtaalamu wa waathirika wa dawa za kulevya, Augustine Godman
Huenda tumewaona wengi wao kama mashujaa, vijana wa kisasa au hata dada zetu wanaokwenda na wakati, kumbe ni wagonjwa wa akili.
Unasikiliza taarifa ya habari jioni. Unasikia
kuwa, mwanamume amembaka mtoto wa miezi mitatu. Unaihoji nafsi yako… ni
jambo gani lililosababisha akafanya ukatili huo? Je, ni tamaa kali ya
ngono?
Wengine hudhani ni kisasi au imani za kishirikina na kwamba wahusika wametumwa.
Huu ni upotoshaji, lakini ukweli ni kuwa hayo ni
magonjwa ya akili ya ngono ambayo yanawakumba asilimia 35 au zaidi ya
Watanzania wote.
Watanzania hawa wanaugua magonjwa haya kwa wakati
mmoja na kusababisha madhara mbalimbali kijamii, kiuchumi na migogoro
katika familia na katika uhusiano.
Watu wenye magonjwa haya, si lazima watembee wakiokota makopo, kuvua nguo au kuwa na nywele ambazo hazijachanwa.
Hawa ni watu wa kawaida ambao tunafanya nao kazi, wenye uwezo mkubwa katika taaluma au pengine ni wazazi au hata walezi.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili na mtaalamu wa
waathirika wa dawa za kulevya, Augustine Godman anasema, magonjwa ya
akili kwa ujumla wake yanaweza kuzidi 1,886 lakini yapo yale ya ngono
ambayo pengine yana changamoto lukuki kwa mwanadamu hasa Watanzania
wasiofahamu kuwa ni magonjwa ya akili.
Dk Godman anafafanua kuwa magonjwa ya akili ya
ngono kuwa ni yale yanayohusisha athari , upungufu au mparaganyiko au
vitu visivyo vya kawaida katika tendo la ngono.
“Mtu anaweza kuwa na matatizo ya kihisia au ya
kisaikolojia au vya kitabia katika suala la ngono na huweza kusababisha
madhara au kutopata mafanikio,” anasema Dk Godman
Daktari huyu ambaye amewahi pia kufundisha Chuo
Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), kitengo cha magonjwa ya
akili anasema watu wengi wana magonjwa ya akili ya ngono, lakini
hawajui kama ni magonjwa na wanaendelea kuishi hivyo hivyo wakidhani
ndivyo walivyo na baadhi wakipata matatizo katika jamii, wengine
kufungwa jela au kupigwa kutokana na tabia hizo.
Mara nyingi tumekuwa tukiona wanawake wanavaa mavazi ya nusu uchi, wakizianika nje sehemu kubwa za miili yao.
Tabia hizo ambazo pengine huweza kuigwa na wengine ni miongoni
mwa magonjwa ya akili ya ngono kwani watu wanaopenda kufanya hivyo
hujisikia raha na amani watu baki au wageni wenye jinsi tofauti
wanapoyaangalia maungo yao na kushtuka.
“Kwa kitaalamu, ugonjwa wa akili ya ngono wa
kupenda kuacha mwili wazi unaitwa ‘exhibitionism’ ambapo mtu huweza
kuamua kuacha maziwa, mapaja au kwa wanaume kuvaa suruali inayoelekea
kuanguka kutoka maungoni,” anasema
Anasema, watu aina hii hutosheka kimapenzi mara tu
wanapoona wanaume au wanawake wengine wameyaona maungo yao. Hata
hivyo, anasisitiza kuwa hutosheka pale tu watu wageni wanapoyaona maungo
yao.
Mhadhiri wa Sosiolojia, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Dk Thomas Ndaluka anasema, baadhi ya magonjwa haya
yanasababishwa na historia ya mtu.
Anasema hata hivyo mparaganyiko kama ule wa
kupenda kuacha maungo wazi, unaambukiza kwa maana ya kuwa, anayeanza
kufanya hivyo ni mgonjwa wa akili na matokeo yake wengine wanaiga.
Chanzo Mwananchi
Chanzo Mwananchi
No comments:
Post a Comment