Wakati Serikali ikiwa katika hatua za utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwenye elimu, imebainika kuwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaohitimu, wanafanya udanganyifu kwenye utafiti kwa kufanyiwa na watu wengine au kununua uliokwisha andikwa.
Kila mwanafunzi anayesomea shahada ya kwanza,
uzamili au uzamivu hutakiwa kufanya utafiti ikiwa ni sehemu ya vigezo
vya kukamilisha masomo yake.
Hata hivyo, Mwananchi imebaini kuwapo kwa
wanafunzi wengi wanaotumia mbinu mbalimbali za kuandika utafiti huo bila
kwenda maeneo husika.
Uchunguzi wetu uliofanyika kwa muda mrefu kwenye
vyuo mbalimbali jijini Dar es Salaam, umebaini kuwa baadhi ya wanafunzi
huchukua tafiti za zamani na kuzinakili upya, huku wengine wakichukua
kutoka kwenye mitandao na kuzifanyia marekebisho kidogo ili zifanane na
eneo analotaka kufanyia utafiti huo.
Mtafiti Mwandamizi ESRF
Mtafiti Mwandamizi, Taasisi ya Utafiti wa Uchumi
na Jamii (ESRF), Dk Donatila Kaino anasema ni asilimia 20 tu ya
wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu nchini, ndiyo wanaoweza kuandika
utafiti kwa ufasaha.
Anasema tatizo hilo linatokana na mfumo wa elimu
uliopo nchini ambao haumpi mwanafunzi nafasi ya kujifunza kuandika
utafiti tangu akiwa shule ya msingi.
“Tatizo kubwa walimu hawafundishi; mtalaa siyo
tatizo sana, kama walimu hawafundishi tangu shule za msingi hadi
sekondari unategemea nini?” an
No comments:
Post a Comment