Malinzi aliyasema hayo jana kwenye hafla ya
uzinduzi wa ushirikiano kati ya klabu hiyo na Kampuni ya Simu za Mkononi
ya Airtel hasa katika maendeleo ya soka ya vijana.
“Ukifika England, waambie wakubwa, benchi la
ufundi kuwa tunawaalika Tanzania kucheza mechi moja, pia kuna mambo
mengi ya kuona huku kuna Mbuga za Wanyama Serengeti, Selou, Manyara,
Mlima Kilimanjaro kuna mengi ya kuvutia,” alisema.
Alisema kuwa kuja kwa timu hiyo itakuwa funzo zuri
kwa maendeleo ya soka kwani vijana watataka kuiona ‘live’ na watacheza
kama wanavyocheza wao.
“Walikuwa Afrika Kusini, waliwahi kwenda Nigeria na hata Tanzania wanaweza kuja...waje,” alisema Malinzi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa
Michezo, Leonard Thadeo alisema hatua ya Manchester United kuunga
urafiki na Airtel itasaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha maendeleo ya
soka ya Tanzania kwa vijana.
“Ni nafasi ya Tanzania kujifunza aina ya soka ya
England kwani walishaanzisha mpango wa Airtel Raising Stars ambao
unatengeneza vipaji kwa vijana...naomba TFF na wadau wengine kuendeleza
vijana hawa.
“Lakini pia mwaka 2015 ni uchaguzi, tuitumie soka
hiyo hiyo kudumisha amani na umoja kwa Watanzania na kwamba Serikali
itakuwa bega kwa bega na TFF katika kushughulikia maendeleo ya soka,”
alisema.
No comments:
Post a Comment