Friday, 28 February 2014
Kurasa za mwanzo na mwisho magazetini leo February 28 2014
Ex-girlfriend wa Samuel Eto’o ashtua watu kuhusu umri wa mchezaji huyo.
“Tatizo la Chelsea ni kukosa wafungaji, nina Eto’o ambaye ana miaka 32 au labda 35 nani anayejua?”.
Hiyo ilikua ni kauli ya kocha Jose Mourinho akimzungumzia Samuel Etoo na baadae mpenzi wa zamani wa Eto’o aliongea kuhusu umri wa mchezaji huyo kitu ambacho kimewashangaza watu wengi.
Anna Barranca alikuwa mpenzi wa zamani wa Eto’o na kupata mtoto mmoja wa kike ambaye hivi sasa ana miaka 11 amesema Eto’o ana miaka 39 kuelekea 40 na sio 35.
Mwanamke huyo amesema kwamba alijua kuhusu umri wa Eto’o wakati wapo Cameroon kutoka kwa mtu ambaye alikua pamoja na Etoo tangu utotoni.
Tuesday, 25 February 2014
James Mapalala:Mwanzilishi wa mageuzi aliyeishia kwenye mikosi.
HARAKATI za mageuzi nchini zina historia ndefu, zikianza kabla
ya uhuru ambapo wa wananchi kupitia vyama na vuguvugu za aina mbalimbali
waliungana ili kuwaondoa wakoloni.
Hadi mwaka 1961 chama cha Tanu kilichokuwa kikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere kilishinda uchaguzi na kuunda Serikali.
Vyama vingine vilivyokuwepo ni pamoja na AMNUT, ANC na UTP.
Baada ya Mwalimu kuunda Serikali, alifanya
mabadiliko kadhaa ambapo mwaka 1965 alifuta mfumo wa vyama vingi na
kukifanya chama cha Tanu kushika hatamu za uongozi.
Mbali na kufutwa kwa mfumo huo, pia uhuru wa
vyombo vya habari na uhuru wa asasi za kiraia ulidhoofishwa huku jumuiya
mbalimbali za kiraia zikichukuliwa na kuwa jumuiya za Tanu.
Hata hivyo, hatua hiyo haikuwafurahisha baadhi ya watu akiwemo James Mapalala ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mwalimu.
Mapambano yalipoanza
Akizungumza maisha yake hivi karibuni, Mapalala
anasema aliamua kupambana na mfumo huo kutokana na ukandamizwaji wa haki
za binadamu uliokuwa ukifanywa na Serikali tangu ngazi za juu hadi
chini.
“Nilianza mapambano yangu rasmi mwaka 1968 wakati
huo nikiandika makala katika Gazeti la Kiongozi wakati huo nikiwa naishi
Tabora. Nilieleza kutoridhishwa na mateso wanayopata wananchi wakati
huo ingawa kwa kweli Mwalimu Nyerere alikuwa na nia njema tu,” anasema
Mapalala na kuongeza:
“Viongozi wa vijiji wakati ule walikuwa wakitesa wananchi na mimi niliandika kila kilichotokea.”
Kutokana na hali hiyo Mapalala alijikuta matatizoni na kufungwa jela katika gereza la Uyui na huo ulikuwa ni mkasa wa kwanza.
“Mkuu wa mkoa wakati huo akiitwa Makinda ambaye ni baba wa spika wa sasa, Anna Makinda, aliniweka jela.
Nilikaa kwa muda fulani hadi maaskofu na mashehe wa mkoa huo
waliponihurumia na kumwandikia barua Mwalimu Nyerere kumwomba nitolewe,”
anasema.
Anasema ombi hilo lilikubaliwa na Mwalimu Nyerere na hivyo kutolewa.
Hapo alifungua ukurasa mwingine ambapo kutokana na
taaluma yake ya ualimu, aliomba na kupata kazi katika Shirika na la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) mwaka 1971.
“Nilitakiwa kwenda kufundisha Nigeria, hivyo
nikaenda kuripoti kisha nikarudi ili niichukue familia yangu.
Niliporudi, Jumapili moja nikiwa kanisani pale St. Peter, Oysterbay
nikakutana na Nyerere… akaniita na kuniuliza, ‘nasikia unataka
kuondoka?’ nikamjibu ni kweli. Akaniambia nisiondoke kuna kazi atanipa,
hivyo niripoti ofisi za Tanu pale Lumumba siku iliyofuata,” anasema.
Anasema siku hiyo alipofika ofisini hapo,
aliwakuta maofisa wa chama ambao walimpangia kazi ya kununua na kuuza
ng’ombe kutoka mikoani.
“Niliifanya kazi ile kwa shingo upande kwa miaka
miwili kisha nikaiacha. Hapo tena ile kazi yangu ya Unesco ikaota
mbawa,” anasema.
Anasema tangu wakati huo alianza kufanya kazi zake
binafsi ikiwa ni pamoja na kuwa mkandarasi wa majengo ambapo anasema
aliwahi kupata zabuni ya kujenga maghorofa ya bandari.
Hata hivyo anasema ilipofika mwaka 1983, mapambano
yake yakaanza tena ambapo wakati huo kulikuwa na mkutano wa wanasheria
jijini Dar es Salaam ambao pia walimkaribisha.
“Wakati huo kulikuwa na wanasheria kutoka katika
Chama cha Tanganyika Law Society walinialika kwenye mkutano uliokuwa
ukizungumzia matatizo ya demokrasia nchini. Walizungumzia matatizo ya
mfumo wa chama kimoja, lakini hawakutoa suluhisho. Mimi nilipendekeza
uanzishwe mfumo wa vyama vingi nchini,” anasema Mapalala.
Hata hivyo, pendekezo hilo halikutiliwa maanani
hadi mwaka 1984 wakati Chama Cha Mapinduzi kikiwa na mkutano mkuu ambapo
Mapalala alifanya tena ‘uchokozi’ wake.
“Mwaka 1984 nilimwandikia barua Mwalimu Nyerere
wakati wa mkutano mkuu wa CCM nikimtaka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama
vingi. Hapo ndipo matatizo yakaanza kwani niliwekwa kizuizini. Nilikuwa
nikihamishwa kutoka kituo kimoja cha polisi hadi kingine kwa karibu
mwaka mmoja. Lakini zikufunguliwa kesi yoyote,” anasema.
Anaongeza kuwa mwaka 1986, aliyekuwa Waziri wa
Mambo ya Ndani, Muhidin Kimario alimkamata na kumfunga minyororo na
kumpeleka kizuizini mkoani Lindi ambako alikaa hadi mwaka 1990 na wakati
huo nilikuwa nikihamishiwa kisiwani Mafia.
Licha ya matatizo yote hayo Mapalala anasema hakukata tamaa na mawazo yake ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi.
“Baada ya kutoka kizuizini, nilirudi tena na
mawazo ya kuanzisha chama cha siasa. Nilikuwa na wenzangu ambapo
tulianzisha chama wakati hakukuwa na sheria ya vyama vingi,” anasema na
kuongeza:
“Hatukuogopa, tulikwenda kwa Waziri wa Mambo ya
Ndani, wakati huo Augustine Mrema na kumweleza haja yetu hiyo. Mrema
alikuwa mkali sana akatufokea na kutufukuza.”
Baada ya kuona hivyo anasema waliamua kuandamana wakidai haki ya kuanzisha chama cha siasa,
“Tulikuwa watu 35 hivi, wakati maandamano yetu
yanaanza. Tulipokuwa tukikaribia Kariakoo, watu waliongezeka na kufika
hadi 1,000. Polisi wakaingilia kati na kuwakamata watu 25, mimi
nikakimbilia Ubalozi wa Sweden kujificha.”
Anaendelea kusema kuwa, wale wanachama
waliokamatwa na kupelekwa mahabusu waligoma kula kwa siku kadhaa na
kuanza kuitisha Serikali.
“Ilibidi Serikali ije kuniomba niwasihi wale
chakula. Ikabidi kitolewe chakula kizuri tena kutoka Kilimanjaro Hotel
na kupelekwa gerezani na kuwabembeleza kula,” anasema.
Wakati mivutano hiyo ikiendelea, tayari
kulishaanza kujitokeza mabadiliko ya kisasa na kiuchumi ulimwenguni
ambapo mfumo wa ukomunisti ulianza kuanguka.
Kuanzisha, kufukuzwa CUF
Baada ya misukosuko ndipo walianzisha chama chao rasmi kikitwa Chama cha Wananchi (CUF) mwaka 1991.
Baada ya Serikali kupitisha sheria ya vyama vingi
mwaka 1992, Mapalala anasema wanaharakati wengine wa mageuzi walikutana
ukumbi wa Diamond Jubilee mwaka huo na kuanzisha chama cha NCCR-Mageuzi.
Hata hivyo, anasema mwaka huo kulikuwa na chama
kingine huko Zanzibar cha ZUF (Zanzibar United Front) ambacho kilitaka
kuunganisha nguvu na chama cha bara ili kiwe cha kitaifa.
“Walipokuja bara kuangalia chama chenye nguvu, wakaridhika na
chama chetu na kuomba tuungane. Halmashauri kuu za vyama vyetu zikakaa
kujadili suala hilo na hatimaye kukubaliana. Mwaka 1993 niliteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa Taifa wa CUF iliyoungana,” anasema.
Baada ya hapo anasema alifanya ziara katika mikoa karibu yote ya bara na Zanzibar kwa ajili ya kukitangaza chama hicho.
Hata hivyo, bahati haikuwa yake, anasema ilipofika
mwaka 1994 mambo yakabadilika kwani wenzake hasa viongozi wa Zanzibar
wakamgeuka na kuanza kumtuhumu kuwa anakisaliti chama.
Lakini mwenyewe anasema ilikuwa ni sababu za kidini pamoja na mkono wa Serikali uliokuwa ukiendelea kumwandama.
“Nilifukuzwa CUF kwa sababu za kidini tu. Ilikuwa
mwaka 1994 baada ya kukijenga chama hicho nikashangaa mambo yamebadilika
na viongozi wenzangu wamenigeuka. Wakawa wananishutumu kuwa natumiwa na
CCM, mara nimechana bendera za chama, na tuhuma nyingi tu. Lakini
nilipata hadi nyaraka zilizothibitisha sababu za udini,” anasema na
kuongeza:
“Wakati huo CUF ilikuwa ikifadhiliwa na nchi za
kiarabu, kwa hiyo wakasema ‘mtatakaje msaada wakati chama kinaongozwa na
kafiri?’ Ndipo vituko vikaanza. Lakini hata Serikali pia ilichangia,
nakumbuka siku ya mkutano wa kunifukuza kule Tanga, Msajili wa vyama vya
siasa wakati huo, George Liundi alikuwepo hadi saa tisa za usiku
akishadadia kufukuzwa kwangu.”
Baada ya kufukuzwa Mapalala akaanza upya tena
mikakati ya kuanzisha chama kingine. Hata hivyo ilimchukua muda mrefu
hadi mwaka 2003 ambapo alianzisha Chama cha Haki na Ustawi alichonacho
hadi sasa.
Tangu alipokianzisha alifanikiwa kupata diwani
mmoja tu mkoani Mara mwaka 2005 ambaye hata hivyo hakuendelea baada ya
kumaliza miaka yake mitano.
Mapalala anazungumzia pia tukio la kunyang’anywa
nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Morocco jijini Dar es Salaam kwa amri
ya mahakama mwaka 2010, na kulihusisha na misukosuko aliyoipata katika
harakati za kuleta mageuzi nchini.
“Hapa unapoona ninaishi kwenye mabanda ya ng’ombe,
baada ya nyumba yangu kubomolewa kwa amri ya mahakama, yaani ni
misukosuko tu. Chama changu kinanitegemea kifedha lakini kwa hali hii
inaniwia vigumu kukisaidia,” anasema.
Anazungumziaje upinzani wa sasa?
Akizungumzia vyama vya upinzani vya sasa, Mapalala
anasema kuwa vimejikita zaidi kwenye kutafuta madaraka badala ya
kueleza sera zao kwa wananchi.“Tofauti kati ya upinzani tuliokuwa tukiupigania miaka ile na wa sasa,
ni watu kuwa na mawazo ya kwenda Ikulu tu bila kusema watawafanyia nini
wananchi baada ya kufika huko. Hata kwenye chama tawala, CCM, hali ni
hiyo hiyo, watu wanalilia tu Ikulu. Sisi tunasisitiza sera tu… sera
nzuri ndiyo zitakazouza chama, chema chajiuza kibaya chajitembeza,”
anasema.
Mwananchi
Mwananchi
Serikali yatangaza nafasi za kazi 1,100
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma imetangaza nafasi za kazi 1,134 katika sekta mbalimbali
za ofisi za umma.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira
katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo
zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ya www.ajira.go.tz
ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.
Katibu alifafanua kuwa nafasi 949 ni kwa ajili ya
waajiri walioainishwa katika ofisi za wizara, halmashauri na nyingine
185 ni za taasisi na wakala mbalimbali za Serikali.
Aidha, amewataka waombaji wote wa fursa za ajira
kufungua matangazo yote mawili ya kazi na kuzingatia masharti ya
Matangazo yote kama yalivyo katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili
kabla ya kutuma maombi yao Aprili 9, 2013.
Daudi alifafanua kuwa waajiri ambao watatoa ajira
hizo ni makatibu wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Wizara ya
Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Wizara ya Kazi na
Ajira na Ofisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo.
Wengine ni Makatibu wakuu Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Wizara ya Viwanda na
Biashara, Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Nishati na Madini,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi,
Wizara ya Maji na Katibu Ofisi ya Rais Maadili.
Wengine ni Makatibu Tawala wa Mikoa ya Kagera,
Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam,
Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora,
Tanga, Katavi na Arusha; pamoja na wakurugenzi wa halmashauri za majiji
na manispaa Mwanza, Iringa, Songea, Shinyanga, Morogoro, Singida,
Kigoma/ Ujiji na Temeke.
Nafasi nyingine ni kwa ajili ya wakurugenzi wa
Halmashauri za Wilaya Mufindi, Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo,
Bukoba, Muleba, Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga,
Tunduru, Ukerewe, Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa na Meatu.
Nyingine ni Wilaya za Shinyanga, Kishapu, Kilosa,
Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli,
Ngorongoro, Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora,
Babati, Mbulu, Simanjiro na Kiteto.
Pia zimo Wilaya za Handeni, Pangani, Kibondo,
Chamwino Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa na Tandahimba pamoja na
halmashauri za miji ya Njombe na Kibaha. Nafasi nyingine ni za Baraza la
Kiswahili la Taifa (Bakita) na Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa).
Nafasi hizo zilizotangazwa zimegawanyika katika
kada zifuatazo; Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta daraja la II – (nafasi 10),
Ofisa Vipimo II – nafasi 6, Mpima Ardhi, daraja la II (nafasi 26),
Mhandisi daraja la II – Ufundi Umeme – Nafasi 9, Ofisa Mipango Miji
daraja la II– nafasi 13 na Mhandisi daraja la II - Ujenzi (Nafasi 16).
Pia wanahitajika wahandisi daraja la II - Maji
(Nafasi 13), Ofisa Misitu daraja la II (nafasi 7), Ofisa wa Sheria
daraja la II – nafasi 3, Mtakwimu daraja la II – nafasi 8 na nyingine
mbalimbali.
Tiketi zinatia najisi soka la Tanzania
MWAKA mpya 2014 ulianza kwa matumaini makubwa
miongoni mwa wadau wa soka kwamba maendeleo yamefikiwa, ambapo
ilitarajiwa Tanzania ianze kutumia tiketi za elektroniki.
Tiketi hizo zilianza kutumika lakini yalikuwa majanga, teknolojia ikakataa au wadau wakashindwa kuiweka inavyotakiwa.
Sintofahamu hiyo imeturudisha kule kule kwenye tiketi za vishina, ambapo kuna wanaofaidi kwa kukaa milangoni.
Nimeambiwa kuna jamaa wana vishina vya mechi
zilizopita baina ya Yanga na Al Ahly na kwamba si ajabu hata mechi ijayo
watavitumia au kurekebisha kidogo tu.
Soka imekuwa sehemu ya kwenda kula na si sehemu ya
kwenda kutumia uzalendo, elimu, ujuzi na maarifa kuhakikisha sekta hii
nayo inakua kiteknolojia na kulifaidisha taifa kiuchumi.
Tiketi za elektroniki ni hatua moja ndogo tu ya
kuendea usasa zaidi, kwa sababu wenzetu huku wanabofya kwenye mtandao wa
kompyuta, kulipia na kupata tiketi. Tutaona baadaye mifumo yao, manufaa
na mapungufu kama yapo.
Kwetu Tanga yalikuwa maafa zaidi maana milango ya
elektroniki haikuwafungulia washabiki waliofika Mkwakwani na inaelezwa
zaidi ya nusu ya washabiki waliingia bure.
Wapo watu hata ndani ya mfumo wa uongozi wa soka
katika klabu, mikoa na ngazi ya taifa wanapendelea mfumo wa kuchana
tiketi pale mlangoni.
Ndiyo maana nachelea kusema kwamba mfuko wa elektroniki umekwama bali labda itakuwa sahihi zaidi kusema umekwamishwa.
Zipo tetesi pia kwamba Wachina walipokuwa
wakijenga Uwanja wa Taifa ambao ni wa kisasa zaidi Afrika Mashariki
walitoa wazo la kuweka mfumo huo moja kwa moja lakini ‘wadau wa
maendeleo’ wakakataa. Kisa? Wanajua wao.
Kwa hali ilivyokuwa mbaya, wakati Ligi Kuu
Tanzania inaanza kuhusiana na suala la tiketi, Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) halikuwa na la kufanya zaidi ya kuzuia matumizi ya tiketi
hizo. Niseme tu kwamba kuna watu waliopinga tangu awali tiketi hizo na
wataendelea kupinga nyingine zozote zenye mfumo wa kuziba mianya ya
wizi.
Wenzetu hapa Uingereza na mataifa mengine
yaliyoendelea kisoka, ambayo hatuna budi kuyaiga katika mazuri yao,
wanaoruhusiwa kuuza tiketi za mechi hapa ni klabu husika tu au mawakala
wao waliopo kisheria na si kuchagua sijui vibanda vya soda au mikate
Mwenge, Tandika au Ilala Bungoni.
Ni kosa kubwa kujihusisha na uuzaji wa tiketi ovyo, lakini kama
ambavyo kuna wachumia tumbo hapo nyumbani, wapo hapa wanaojaribu kuzi
upload tiketi kwenye tovuti mbalimbali na baadhi hudiriki kwenda karibu
na viwanja na kuziuza kwa bei ya juu.
Bodi ya Ligi Kuu (Premier League) hapa England
wamekuwa wakali sana wakishirikiana na mamlaka za dola kupambana kwa
mafanikio makubwa na wauzaji feki wanaotundika tiketi kwenye tovuti na
kuziuza na pia watu kadhaa wamedakwa na kushitakiwa kwa kuzilangua
viwanjani.
Hili, pengine sawa na linaloweza kuwa limetokea au
litatokea nyumbani, linakwenda sambamba na uuzaji wa tiketi za
kughushi, ndiyo maana kama kuna kitu kinasisitizwa sana kwenye nchi hizi
ni kununua tiketi (na bidhaa nyingine zozote) kwa mhusika halali na
kupata stakabadhi.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaposisitiza
ukinunua dai stakabadhi na ukiuza toa stakabadhi, ni jambo ambalo huku
ni la lazima, hata kama hutaki utajikuta umechanganyiwa stakabadhi ama
na bidhaa zako au na chenji.
Klabu mwenyeji huuza tiketi zake lakini huwawekea
wageni idadi wanayokubaliana na hutolewa mapema, iwe ni mechi ya Ligi
Kuu au ya kimataifa na wala hutaona mkanganyiko.
Tiketi zikisemwa zimeisha basi shabiki ambaye
angetaka kwenda uwanjani anashauriwa abaki nyumbani, atazame kwenye
televisheni na kuwahi kutazama mtandaoni ratiba ya mechi inayofuata
anunue mapema tiketi yake awe nayo kibindoni.
Malalamiko ambayo yamepata kuwapo ni tiketi za
baadhi ya mechi kuwa ghali sana, mojawapo ya klabu zenye aina hiyo ni
Arsenal lakini watu wanaoingia Emirates ni karibu 60,000.
Bodi ya EPL kwa mfano, imekuwa ikisambaza
matangazo kwa njia mbalimbali kuwaasa washabiki walio ng’ambo ambao
wangependa kuingia England kutazama mechi za EPL kuwasiliana kwanza na
klabu husika kwenye tovuti zao.
Ni tofauti kabisa na jamaa wa Mbeya City
wanaopanda Coaster zao na kutinga Dar kwa ajili ya mechi dhidi ya Simba
siku hiyo hiyo ya mechi pasipo kuwa na tiketi mkononi, maana watazipata
tu uwanjani na wanasema uwanja haujai, kwani eti si sawa na ndoo ya
maji.
Premier League pia inatoa angalizo kwa washabiki
hao, hasa wa ng’ambo kupendelea zaidi kununua tiketi kutoka kwa klabu
husika ili kujiridhisha kwamba ni halali.
Ununuzi wote huo ni kwa mtandao, ambao rafiki zangu wa Tanzania watakuwa hawaupendi.
Tiketi za mechi za EPL zina soko sana kutokana na
washabiki wengi kupenda kwenda wenyewe uwanjani kujionea mechi na
wachezaji wawapendao, hata kwa kusafiri umbali mrefu.
I.G.Saria,
M: +44 (0) 7791284317
E: saria@tanzaniasports.com
Tunachojidanganya kuhusu Kaseja na Dida
SAYANSI ya soka la Tanzania ni tofauti na sayansi ya soka lolote
ulilowahi kusikia duniani. Kuna wakati unajaribu kujiuliza tunatumia
sayansi gani katika soka la kisasa lakini unaishia kukosa jibu.
Kwa mara ya kwanza nimesikia kuwa Tanzania kuna
kipa wa mechi za ndani za ligi, na kuna kipa wa mechi za kimataifa.
Hauwezi kuipata hii kokote duniani. Zamani na hata sasa tulizoea kusikia
kipa wa dakika 90 na kipa wa kuja kucheza penalti baada ya dakika 120.
Lakini kuna sayansi mpya ya kipa wa mechi za
kimataifa na kipa wa mechi za ndani. Ndivyo wanavyojidanganya watu wa
benchi la ufundi au viongozi wa Yanga. Kwamba Juma Kaseja ni kipa
waliyemsajili kwa ajili ya mechi za kimataifa wakati Deogratius Munishi
‘Dida’ ni kipa waliyemsajili kwa ajili ya mechi za ndani.
Katika soka halisi hakuna kitu kama hiki. Kipa wa
mechi za ndani anapaswa kucheza mechi za kimataifa kwa sababu anacheza
mechi nyingi kila mwisho wa wiki na ni rahisi kuwa fiti kuliko kipa wa
mechi za kimataifa.
Kipa wa mechi za kimataifa anacheza mechi nne au
sita tu kwa mwaka. Tangu lini kipa akacheza mechi chache kama hizi na
akawa fiti kama si kumtafutia lawama?
Na hii si kwa kipa tu, bali kwa mchezaji yoyote uwanjani.
Kama Yanga wanataka kufanya vizuri katika mechi
zao za kimataifa ni bora waendelee kumtumia Dida kwa sababu wakimtumia
Kaseja watajikuta wanamlaumu bila ya sababu za msingi kwani naye
anahitaji mazoezi yenye ushindani ili kulinda kipaji chake jambo ambalo
kwa sasa analikosa .
Na kama wanataka Kaseja awe kipa wa mechi za
kimataifa, basi huu ni wakati wa kuanza kumpanga mechi za ndani ili
aendelee kuchangamka langoni.
Barani Ulaya, kipa wa kwanza anabakia kuwa kipa wa
kwanza tu kwa sababu kadri anavyokumbana na mikikimikiki langoni ndivyo
anavyoendelea kuimarika.
Kadri kipa yeyote anavyokaa nje ndivyo anavyoendelea kuporomoka kiwango chake taratibu bila ya kujifahamu.
Katika pambano la Jumamosi dhidi ya Al Ahly
natazamia Kaseja kutocheza vema kama akipangwa kwa sababu uzoefu pekee
hausaidii kiwango kizuri cha mchezaji.
Mikikimikiki ya kila wiki inasaidia zaidi wachezaji hasa wa nafasi ya kipa. Kwa mshambuliaji haliwi tatizo kubwa sana.
Sir Alex Ferguson aliwahi kutaka kuwabadili makipa wake, David
de Gea na Anders Lindergaard kadri awezavyo lakini mwisho wa siku
alilazimika kukubali ukweli kwamba De Gea angecheza mechi karibu zote za
Manchester United akiwa chaguo namba moja katika kikosi cha kwanza.
Na labda kwa ushauri mwingine kwa watu wa Yanga ni
kwamba hawana sababu yoyote ya kumuharibia maisha kipa wao wa tatu,
Ally Mustapha ‘Barthez’.
Huu ni wakati mwafaka wa kumruhusu kipa huyo
aondoke klabuni kwao hata kama ana mkataba nao. kwani hawamtumii na
hivyo anahitaji changamoto kupitia klabu nyingine ambazo zinahitaji
huduma yake.
Kwa eneo la golikipa, daima unapaswa kuwa na
makipa wawili wakubwa kama Dida na Kaseja. Kipa wa tatu anapaswa kuwa
kipa kijana ambaye atakuwa ana maisha marefu klabuni huku akijifunza
kutoka kwa wawili waliopo.
Kwa ilivyo sasa, Barthez hana cha kujifunza kutoka
kwa Kaseja wala Dida. Hapo hapo unajaribu kuwaza kuwa kama Kaseja
anasugua benchi vipi kwake yeye? Uungwana mzuri sana ni kumruhusu
aondoke kwenda kucheza katika timu ambayo atapangwa mara kwa mara.
Mwanaspoti
Mwanaspoti
Al Ahly yakodi mpishi Mjerumani
KIKOSI cha timu ya soka ya Al Ahly ya Misri, kitafikia kwenye
hoteli ya kifahari ya Kempinski jijini Dar es Salaam, lakini kwenye
msafara wao watakuja na mpishi wao maalumu.
Timu hiyo ya Misri imepanga kutua Dar es Salaam
leo Jumanne ingawa haijawapa taarifa Yanga na tayari maofisa wao wapo
jijini wakiandaa mazingira.
Hata hivyo timu hiyo imezuga kwenye mitandao yao
kwamba hawako vizuri kiuchumi kwa sasa na kwamba hata Sh112 milioni
walizotumia kwa safari ya kuja nchini wamezipata kwa kuungaunga.
Al Ahly inayowasili na msafara wa watu 32 miongoni
mwao wachezaji wakiwa 22 na viongozi 10, mpishi wao ni raia wa
Ujerumani ambaye atashirikiana na wataalamu wa hoteli hiyo.
Timu hiyo ilizikataa hoteli tano za awali
ilizotafutiwa na Yanga kwa madai kwamba zina vyumba vidogo. Ikiwatumia
maofisa kadhaa wa ubalozi wa Misri nchini, Al Ahly iliamua kuchagua
hoteli hiyo huku ikipata uwanja wa mazoezi katika Shule ya Kimataifa ya
Tanganyika (IST), Masaki sehemu ambayo ina ulinzi mkali na mashabiki
hawaingii kirahisi.
Mkurugenzi wa Michezo wa Al Ahly, Sayyid Abdul
Hafiyz, alitarajiwa kuwasili jana Jumatatu kuungana na maofisa wengine
waliotangulia.
Viongozi wa Simba wamepata msiba wa mjomba yupi?
UMEWAHI kuona rubani anaiteka ndege yake? Bila shaka unakumbuka
kisa cha rubani msaidizi, Hailemedhin Abera (31) aliyeiteka ndege ya
Ethiopian Airlines Jumatatu ya wiki iliyopita kwa madai ya kuwa na
msongo wa mawazo kwa kufiwa na mjomba wake.
Abera, ambaye amefanya kazi kwenye shirika hilo
maarufu la ndege kwa miaka mitano alijifungia kwenye chumba cha marubani
baada ya rubani mkuu kwenda msalani.
Rubani huyo msaidizi ‘aliendesha’ ndege hiyo kwa
saa sita na badala ya kuipeleka Roma, Italia aliipeleka Geneva, Uswisi
ambako alitua baada ya kuomba kupewa hifadhi nchini humo.
Rubani huyo alifanya kituko kwa kuwatisha abiria
kwa kuchomoa vikasha vya hewa ya oksijeni kwenye ndege hiyo na kutishia
kuzima mfumo wa hewa iwapo abiria hao wasingekubali kufuata maelekezo
yake.
Rubani huyo akawaambia abiria kwa ukali: “Kaeni
chini, vaeni vikasha vya oksijeni kwenye viti vyenu, nitakwenda kukata
mfumo wa hewa ya Oksijeni.”
Baada ya rubani huyo kuwazungusha abiria kwa saa
sita angani wakiwa hawajui hatima yao, alitua Geneva na kushuka kupitia
dirishani kwa msaada wa kamba huku akiomba hifadhi kabla ya
kujisalimisha kwa polisi.
Ndege hiyo aina ya Boeing 767-300 iliyokuwa na
abiria 201 na wahudumu iliondoka mjini Addis Ababa na kutua mjini
Geneva, ikiwa imebakiza mafuta yanayayoiwezesha kuendelea kuwepo hewani
kwa dakika 20 tu.
Si ndege tu ambayo inaweza kutekwa, hata viongozi
wa Simba wamewateka nyara wanachama wao kwa kuitisha mkutano mkuu Machi
16 ambao utajadili ajenda moja tu ya mabadiliko ya katiba.
Itakuwaje Simba yenye migogoro mingi iwe na ajenda
moja tu ya kujadili mabadiliko ya katiba wakati wanachama wanataka
kujua suala la uwanja wao wa Bunju B.
Itakuwaje ijadiliwe ajenda moja tu katika mkutano
huo wakati wapo baadhi ya wanachama katika Simba ambao wanataka kujua
Emmanuel Okwi aliuzwa vipi kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia bila
malipo yoyote.
Wanachama wanataka kupata majibu inakuwaje Okwi licha ya ubora wake auzwe kwa mkopo na fedha haijalipwa mpaka sasa?
Wanachama wanataka kujua inakuwaje mchezaji wao
kiraka Shomari Kapombe apelekwe AS Cannes ya Ufaransa kwa mkataba ambao
hauna maelezo ya kujitosheleza.
Kapombe, miongoni mwa wachezaji bora Afrika Mashariki na Kati sasa yupo nchini akiwa hajui hatima yake, lakini Simba wapo kama vile hawana shida naye.
Kapombe, miongoni mwa wachezaji bora Afrika Mashariki na Kati sasa yupo nchini akiwa hajui hatima yake, lakini Simba wapo kama vile hawana shida naye.
Simba imecheza mechi nne na kupata pointi mbili
tu, kuna tatizo gani hapo. Wanachama wanataka kupata majibu sahihi kuna
tatizo gani katika timu hiyo?
Matatizo yote hayo yanapaswa kujadiliwa katika
mkutano mkuu wa wanachama wa Simba na hasa ikizingatiwa kuwa kuna
mgawanyiko mkubwa ndani ya uongozi na Kamati ya Utendaji.
Kwa misimu miwili mfululizo, Simba inashindwa
kushiriki mashindano ya Shiriisho la Soka Afrika (CAF) iwe Ligi ya
Mabingwa au Kombe la Shirikisho. Wanachama wanataka kujadili hayo.
Inawezekana Simba inataka kufika mahali fulani
kuzuri, lakini viongozi wake wamewateka wanachama na wanawapeleka sehemu
nyingine huku wakiomba hifadhi maalumu.
Yule rubani wa Ethiopia aliiteka ndege kwa madai
alikuwa na msongo wa mawazo baada ya kufiwa na mjomba wake, sielewi
viongozi wa Simba wamepata msongo wa mawazo baada ya kufiwa na mjomba
yupi?
Mwanaspoti
Mwanaspoti
Yanga, Simba milioni 100
MECHI za Ligi Kuu Bara zilizohusisha Yanga na Simba na kuchezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wikiendi iliyopita zimeingiza Sh101
milioni.
Yanga ambayo Jumamosi iliyopita iliichapa Ruvu
Shooting mabao 7-0 mechi yake iliingiza Sh68.4 milioni kutokana na
mashabiki 11,972 kuingia uwanjani.
Katika mechi hiyo kila klabu ilipata mgawo wa
Sh15,687,488 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa
kutokana na mapato hayo ni Sh 10.4 milioni. Gharama za tiketi ni Sh3.8
milioni na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilipata Sh 4.8 milioni
wakati uwanja ulipata Sh8.1 milioni.
Gharama za mchezo zilikuwa Sh4.8 milioni wakati
Mfuko wa Maendeleo ya soka (FDF) Sh2.4 milioni. Chama cha Soka Dar es
Salaam (DRFA) na Chama cha Soka Pwani (COREFA) kila kimoja kilipata
Sh945,110.
Simba na JKT Ruvu iliyochezwa juzi Jumapili na
kushuhudiWa na watazamaji 5,850 iliingiza Sh32.7 milioni kwa viingilio
vya Sh5,000, Sh 15,000 na Sh20,000. VAT iliyolipwa ni Sh4.9 milioni.
Kila klabu ilipata mgawo wa Sh7.4 milioni, tiketi
ni Sh2.5 milioni huku gharama za mechi zikiwa Sh 2.2 milioni. Uwanja
ulipata Sh3.7 milioni wakati TPLB walipata Sh2.2 milioni. Mgawo mwingine
ni FDF Sh1.1 milioni na DRFA Sh881,376.
Monday, 24 February 2014
VYUO VIKUU 100 BORA AFRICA
1 Cairo University
Egypt
2 University of Cape Town
South Africa
3 University of Pretoria
South Africa
4 Universiteit Stellenbosch
South Africa
5 University of South Africa
South Africa
6 University of the Witwatersrand
South Africa
7 University of the Western Cape
South Africa
8 Ain Shams University
Egypt
9 Alexandria University
Egypt
10 Mansoura University
Egypt
11 University of KwaZulu-Natal
South Africa
12 University of Dar es Salaam
Tanzania
13 The American University in Cairo
Egypt
14 Rhodes University
South Africa
15 Assiut University
Egypt
16 Université Mohammed V – Agdal
Morocco
17 University of Nairobi
Kenya
18 Université de Ouagadougou
Burkina Faso
19 University of Johannesburg
South Africa
20 Makerere University
Uganda
21 University of Botswana
Botswana
22 Zagazig University
Egypt
23 University of Ghana
Ghana
24 Universidade Eduardo Mondlane
Mozambique
25 Obafemi Awolowo University
Nigeria
26 University of Khartoum
Sudan
27 Université Mentouri de Constantine
Algeria
28 Université de la Reunion
Reunion
29 Benha University
Egypt
30 The German University in Cairo
Egypt
31 Université Cheikh Anta Diop
Senegal
32 Addis Ababa University
Ethiopia
33 North-West University
South Africa
34 Sudan University of Science and Technology
Sudan
35 Université Abou Bekr Belkaid Tlemcen
Algeria
36 University of Namibia
Namibia
37 Al Akhawayn University
Morocco
38 College of Arts and Social Sciences, University of Rwanda
Rwanda
39 University of Lagos
Nigeria
40 Helwan University
Egypt
41 Université Mouloud Maameri de Tizi Ouzou
Algeria
42 Université de Batna
Algeria
43 Nelson Mandela Metropolitan University
South Africa
44 University of Zimbabwe
Zimbabwe
45 University of Zambia
Zambia
46 Université Abdelhamid Ibn Badis Mostaganem
Algeria
47 Université Abdelmalek Essadi
Morocco
48 Université d’Alger
Algeria
49 Université d’Antananarivo
Madagascar
50 Moi University
Kenya
51 Université Mohammed V – Souissi
Morocco
52 South Valley University
Egypt
53 Minia University
Egypt
54 Tanta University
Egypt
55 Al-Azhar University
Egypt
56 Cape Peninsula University of Technology
South Africa
57 University of Ilorin
Nigeria
58 Minoufiya University
Egypt
59 Université M’hamed Bouguerra de Boumerdes
Algeria
60 Université d’Oran
Algeria
61 Suez Canal University
Egypt
62 Kwame Nkrumah University of Science and Technology
Ghana
63 Université Cadi Ayyad
Morocco
64 Federal University of Technology, Minna
Nigeria
65 University of Swaziland
Swaziland
66 Université Ibn Tofail
Morocco
67 Strathmore University
Kenya
68 Université Hassan II Mohammedia – Casablanca
Morocco
69 Kafr el-Sheikh University
Egypt
70 University of Ibadan
Nigeria
71 Université Hassan II – Casablanca
Morocco
72 University of Malawi
Malawi
73 Université des Sciences et de la Technologie Houari Boumediène
Algeria
74 Universiteit van die Vrystaat
South Africa
75 University of Nigeria
Nigeria
76 Universidade de Cabo Verde
Cape Verde
77 Polytechnic of Namibia
Namibia
78 Kenyatta University
Kenya
79 Libyan International Medical University
Libya
80 Ahmadu Bello University
Nigeria
81 University of Mauritius
Mauritius
82 Sirte University
Libya
83 Tshwane University of Technology
South Africa
84 University of Benin
Nigeria
85 University of Agriculture, Abeokuta
Nigeria
86 Durban University of Technology
South Africa
87 Université Kasdi Merbah de Ouargla
Algeria
88 Université de Sousse
Tunisia
89 Université de Tunis El Manar
Tunisia
90 University of Gezira
Sudan
91 University of Cape Coast
Ghana
92 Université de la Manouba
Tunisia
93 United States International University
Kenya
94 Covenant University
Nigeria
95 Central University of Technology
South Africa
96 Université Mohamed Khider de Biskra
Algeria
97 Madonna University
Nigeria
98 The British University in Egypt
Egypt
99 University of Fort Hare
South Africa
100 Sokoine University of Agriculture
Tanzania
Subscribe to:
Posts (Atom)