Monday 3 February 2014

Mbeya City na Yanga zaingiza Sh175milioni, zaambulia Sh84milioni

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Yanga na Mbeya City iliyofanyika jana Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza sh. 175,285,000.fedha hizo zimetokana Watazamaji 30,411 waliokata tiketi kushuhudia mtanange huo.
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 26,738,389.83, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,919,200 wakati kila klabu ilipata sh. 42,960,086.50.
Uwanja sh. 21,844,111.53, gharama za mechi sh. 13,106,466.92, Bodi ya Ligi sh. 13,106,466.92, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 6,553,233.46 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 5,096,959.36

No comments:

Post a Comment