Friday 14 February 2014

Pistorius ajutia kifo cha mpenzi wake

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amezungumzia masikitiko na majuto yake kuhusu mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp, mwaka mmoja uliopita.
Katika taarifa kwa mtandao wake, alisema: ''Kumpoteza Reeva kulinipa huzuni mkubwa sana siku hiyo na nitaubeba maisha yangu yote.''
Kesi ya mauaji dhidi ya Pistorius inatarajiwa kuanza mjini Pretoria mnamo mwezi Machi.
Oscar anasema kuwa alimpiga risasi Reeva kwa bahati mbaya baada ya kudhani kuwa alikuwa jambazi ndani ya nyumba yake alipompiga risasi kupitia mlango wa bafu yake mwaka 2013.
Mwendesha mkuu wa mashitaka anadai kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kupangwa baada ya wawili hao kuzozana.
Huenda akafungwa jela maisha ikiwa atapatikana na hatia.

No comments:

Post a Comment