Tuesday 25 February 2014

Yanga, Simba milioni 100

MECHI za Ligi Kuu Bara zilizohusisha Yanga na Simba na kuchezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wikiendi iliyopita zimeingiza Sh101 milioni.
Yanga ambayo Jumamosi iliyopita iliichapa Ruvu Shooting mabao 7-0 mechi yake iliingiza Sh68.4 milioni kutokana na mashabiki 11,972 kuingia uwanjani.
Katika mechi hiyo kila klabu ilipata mgawo wa Sh15,687,488 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni Sh 10.4 milioni. Gharama za tiketi ni Sh3.8 milioni na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilipata Sh 4.8 milioni wakati uwanja ulipata Sh8.1 milioni.
Gharama za mchezo zilikuwa Sh4.8 milioni wakati Mfuko wa Maendeleo ya soka (FDF) Sh2.4 milioni. Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) na Chama cha Soka Pwani (COREFA) kila kimoja kilipata Sh945,110.
Simba na JKT Ruvu iliyochezwa juzi Jumapili na kushuhudiWa na watazamaji 5,850 iliingiza Sh32.7 milioni kwa viingilio vya Sh5,000, Sh 15,000 na Sh20,000. VAT iliyolipwa ni Sh4.9 milioni.
Kila klabu ilipata mgawo wa Sh7.4 milioni, tiketi ni Sh2.5 milioni huku gharama za mechi zikiwa Sh 2.2 milioni. Uwanja ulipata Sh3.7 milioni wakati TPLB walipata Sh2.2 milioni. Mgawo mwingine ni FDF Sh1.1 milioni na DRFA Sh881,376.

No comments:

Post a Comment