Tuesday 25 February 2014

Al Ahly yakodi mpishi Mjerumani

KIKOSI cha timu ya soka ya Al Ahly ya Misri, kitafikia kwenye hoteli ya kifahari ya Kempinski jijini Dar es Salaam, lakini kwenye msafara wao watakuja na mpishi wao maalumu.
Timu hiyo ya Misri imepanga kutua Dar es Salaam leo Jumanne ingawa haijawapa taarifa Yanga na tayari maofisa wao wapo jijini wakiandaa mazingira.
Hata hivyo timu hiyo imezuga kwenye mitandao yao kwamba hawako vizuri kiuchumi kwa sasa na kwamba hata Sh112 milioni walizotumia kwa safari ya kuja nchini wamezipata kwa kuungaunga.
Al Ahly inayowasili na msafara wa watu 32 miongoni mwao wachezaji wakiwa 22 na viongozi 10, mpishi wao ni raia wa Ujerumani ambaye atashirikiana na wataalamu wa hoteli hiyo.
Timu hiyo ilizikataa hoteli tano za awali ilizotafutiwa na Yanga kwa madai kwamba zina vyumba vidogo. Ikiwatumia maofisa kadhaa wa ubalozi wa Misri nchini, Al Ahly iliamua kuchagua hoteli hiyo huku ikipata uwanja wa mazoezi katika Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Masaki sehemu ambayo ina ulinzi mkali na mashabiki hawaingii kirahisi.
Mkurugenzi wa Michezo wa Al Ahly, Sayyid Abdul Hafiyz,   alitarajiwa kuwasili jana Jumatatu kuungana na maofisa wengine waliotangulia.

No comments:

Post a Comment