Monday 10 February 2014

Taswira ya Tanzania yachafuka nchini Uingereza kwa ujangili

Amini usi Amini huyu jamaa wa kwenye picha ndio yule muwaji ndugu zetu watanzania wenzetu tisa kule tarime . Kwa masikitiko makubwa na simazi tele toka kwa mwanadam yoyote mwenye roho ya ubinaadam na upendo lazima swala zima la mauwaji ya tarime la wanachi na watoto walio uliwa bila sababu ya msingi litakuwa limekugusa na bado limeacha jeraha kubwa kwa ndugu jamaa na familia za marehem kwakuwa walio pigwa risasi na kupoteza maisha yao hakuna baya lolote walilo fanya paka kiasi cha kukatishiwa uhai wao bila sababu zamsingi . Huyu muwaji hivi sasa yupo mikononi mwa jeshi la polisi wa tanzania kwa mtazamo wako je unadhani adhabu gani stahiki inamfaa kwa vitendo vyake vya mauwaji alivyo fanya
- See more at: http://onelovetz.blogspot.com/2014/02/breakin-newzz-hatimaye-yule-mwanaume.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FhgdRs+%28Onelove+Tz%29&utm_content=FaceBook#sthash.WRjVp7pc.dpuf
 Wakati Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kwenda London Uingereza kuhudhuria mkutano wa kuokoa viumbe vilivyo hatarini kutoweka duniani ukianza wiki hii, tatizo la ujangili limeweka wingu zito kwa Tanzania.
Rais Kikwete ni kati ya viongozi wa nchi 50 watakaohudhuria mkutano huo, utakaokuwa chini ya wenyeji wa mwana wa Wales na Waziri wa Mkuu wa Uinegerza, David Cameron,
Taarifa ya gazeti la The Mail on Sunday la Uingereza la Februari 8, limeitaja Tanzania kama kinara wa ujangili kwa kuua zaidi ya tembo 11,000 kwa mwaka, huku Rais wake (Jakaya Kikwete) akielezwa kufumbia macho.
Pia, gazeti hilo limemhusisha Rais Kikwete kuwa na urafiki na wafanyabiashara ya meno ya tembo, huku likiwahusisha wafadhili wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika biashara hiyo.
“Utawala wa Rais Kikwete umetawaliwa na mauaji ya tembo yaliyovunja rekodi katika historia ya nchi yake. Kibaya zaidi, wahifadhi wanasisitiza kuwa, ndani ya Serikali kuna viongozi wanaoshiriki biashara hiyo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Katika mkutano huo, viongozi wa nchi 50 na mawaziri wataweka mikakati dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori, yenye thamani ya pauni 6 bilioni za Uingereza kwa mwaka zinazotumika kufadhili magaidi.
Taarifa hiyo inasema kuna wafanyabiashara wakubwa wa Dar es Salaam wanaohusika na ujangili.
“Miongoni mwao ni  matajiri wakubwa nchini, wafadhili na wanachama wa CCM na ndugu wa karibu wa Rais Kikwete. Lakini wanao marafiki wakubwa, huku majaji, waendesha mashtaka na polisi hurubuniwa kwa urahisi,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Pia, taarifa hiyo inadai kuwapo kwa idadi kubwa ya Wachina wanaofanya biashara ya mafuta nchini, huku baadhi yao wakihusika na ujangili.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu alikiri kuona taarifa hiyo na kwamba, Rais Kikwete atahudhuria lakini aliipuuza taarifa hiyo.
“Ni kweli Rais Kikwete atahudhuria huo mkutano, lakini taarifa ni ya None sense, crap and malicious (ya kishenzi, kipuuzi na ovu),” alisema Rweyemamu.

Mwananchi.
Kuhusu CCM taarifa hiyo imeitaja idara ya wanyapori kunuka rushwa huku ikisingizia kuuzwa kwa meno ya tembo yaliyoko ghalani kwenye soko la kimataifa wakati lengo lao ni kupata fedha kuisaidia chama hicho  uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“ Wabunge, maofisa wa juu na wafanyabiashara, wametajwa bungeni na kwenye vyombo vya habari, lakini uchunguzi unapotezwa,” inaongeza.

Amini usi Amini huyu jamaa wa kwenye picha ndio yule muwaji ndugu zetu watanzania wenzetu tisa kule tarime . Kwa masikitiko makubwa na simazi tele toka kwa mwanadam yoyote mwenye roho ya ubinaadam na upendo lazima swala zima la mauwaji ya tarime la wanachi na watoto walio uliwa bila sababu ya msingi litakuwa limekugusa na bado limeacha jeraha kubwa kwa ndugu jamaa na familia za marehem kwakuwa walio pigwa risasi na kupoteza maisha yao hakuna baya lolote walilo fanya paka kiasi cha kukatishiwa uhai wao bila sababu zamsingi . Huyu muwaji hivi sasa yupo mikononi mwa jeshi la polisi wa tanzania kwa mtazamo wako je unadhani adhabu gani stahiki inamfaa kwa vitendo vyake vya mauwaji alivyo fanya
- See more at: http://onelovetz.blogspot.com/2014/02/breakin-newzz-hatimaye-yule-mwanaume.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FhgdRs+%28Onelove+Tz%29&utm_content=FaceBook#sthash.WRjVp7pc.dpuf

No comments:

Post a Comment