KOCHA Mfaransa, Patrick Liewig, atakuwa jukwaani leo Jumatatu
kuishuhudia Simba na Azam, lakini atakuwa na raha kwani uongozi wa Simba
umemhakikishia kwamba keshokutwa Jumatano atakuwa tajiri kwa vile
watamjaza manoti yake.
Kwa mujibu wa Liewig ambaye yupo Dar es Salaam kwa
siku kadhaa sasa, anaidai Simba Sh26 milioni na amesema Mwenyekiti wa
Simba, Ismail Aden Rage, amemthibitishia kwamba siku hiyo mambo yake
yatakuwa freshi.
Liewig ambaye amegoma kuondoka Dar es Salaam mpaka
atakapopata mshiko wake, alisema: “Nashukuru kuwa tumekubaliana na
Simba kupitia kwa Ismail Rage na Zacharia Hans Pope kuwa watanilipa pesa
zangu kama tulivyoandikishana awali.
“Natarajia mambo yaenda kama yalivyopangwa, ni vizuri kufikia mwisho.”
Liewig aliwasili Dar es Salaam Oktoba 18 na
kushuhudia mchezo wa Simba na Yanga uliofanyika siku mbili baadaye
uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3, Simba ikirudisha yote kipindi cha
pili.
Kocha amesema akishapewa chake, atakwea pipa kurudi kwao.
Hata hivyo kuna habari kuwa anaitamani sana kazi
ya kuinoa Coastal Union na amekuwa akitafuta upenyo wa kuwashawishi
vigogo wa timu hiyo wampe kazi.
No comments:
Post a Comment