NANI KIPA WA KIHISTORIA SIMBA SC Mohamed Mwameja || Juma Kaseja
JUMA
Kaseja alijiunga na Simba SC mwaka 2003, akitokea Moro United na
aliidakia klabu hiyo hadi msimu wa 2009, aliposaini Yanga kwa mkataba wa
mwaka mmoja.
Baada ya makataba wake kwisha, hakuongezewa mwingine na mara moja Simba ikamsajili tena.
Kaseja kwa mara ya kwanza Simba alisajiliwa msimu ambao Mohamed Mwameja
alikuwa amestaafu, akapatikana shujaa mpya wa kwenye milingoti
Msimbazi, mtoto wa Kigoma, aliyekulia Morogoro, Juma K. Juma aka Juma
Kaseja.
Kaseja pia, akiwa Simba katika msimu wake wa kwanza tu
aliifikisha timu hiyo fainali ya Kombe la Kagame nchini Uganda, ambako
walifungwa 1-0 kwa tabu na wenyeji SC Villa.
Msimu huo huo wa 2003,
Kaseja aliiongoza Simba kuitoa Zamalek ya Misri katika Ligi ya Mabingwa
Afrika na kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo, miaka 10 tangu
Mwameja aiongoze Simba kucheza fainali ya Kombe la CAF na kufungwa na
Stella Abidjan.
Kuanzia mwaka 2004, baada ya zama za Manyika Peter, Kaseja akawa Tanzania One na hadi leo - nani mwingine zaidi yake?
Kaseja amepitia vipindi vigumu pia, kuna wakati mwaka 2007
alisimamishwa Simba kwa tuhuma za utovu wa nidhamu, mambo ambayo
yanakatisha tamaa na wakati mwingine yanaweza kukuondoa kwenye soka,
lakini alisimama imara na alipomaliza kutumikia adhabu yake, ameendelea
kuwa Simba One.
Timu ya taifa, alipokuja Mbrazil Marcio Maximo
alimtema kwa sababu hizo hizo za nidhamu na hakumrejesha hadi
alipoondoka na kuajiriwa kocha mpya Mdenmark, Jan Bolrge Poulsen
akamrejesha kikosini.
Alirejea kwa kishindo mwaka 2010, akiiwezesha
timu ya Bara kutwaa Kombe la Challenge ambalo Mwameja alilitwaa mara
moja tu, 1994 nchini Kenya.
Mwameja alitwaa mataji 16 akiwa na
Simba, ambayo ni ubingwa wa Ligi Kuu (matatu) 1994, 1995 na 2001, Kombe
la Nyerere (mawili) 1995 na 2000, Ligi ya Muungano (matano) 1993, 1994,
1995, 2001 na 2002, Kombe la Tusker (mawili) 2001 na 2002, Kombe la
Kagame (manne) 1992, 1995, 1996 na 2002 na kucheza fainali ya CAF 1993.
Kaseja hadi sasa amekwishatwaa mataji sita akiwa na Simba, ubingwa wa
Ligi Kuu Bara 2003, 2004, 2007 na 2010, jumlisha wa 2009 aliotwaa na
Yanga, Kombe la Tusker 2003 na 2005 mawili pamoja la Kenya. Jumla Kaseja
ana Medali nane za dhahabu kabatini kwake.
Tuhuma za kuihujumu
Simba kwenye mechi za Yanga wote wawili zimewakumba - na Kaseja na
Mwameja pamoja na kwamba klabu hiyo wamepitia makipa wengine hodari kama
Omar Mahadhi, Athumani Mambosasa na Father Pazi kati yao unaweza
kumpata kipa bora wa klabu daima.
No comments:
Post a Comment