MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage, amesema hatogombea tena uongozi katika klabu hiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza na Mwanaspoti juzi Jumanne, Rage,
alisema kwamba ameshangazwa na hatua ya baadhi ya watu wanaotaka uongozi
kuanza harakati hizo kwa kuihujumu timu.
Alisema anajua watu hao wanamhofia yeye na ndio
maana wameamua kuanza mapema mikakati yao ya kuwania uongozi kwa
kuihujumu klabu wakiamini ndio njia ya kummaliza, lakini amewatoa hofu
kwa kusema yeye hatogombea.
“Ninapenda niwaambie wanaonihofia kuwa, sitagombea
tena. Lakini napenda pia kusema kuwa wanaotaka uongozi wajue kwamba
zama za uongozi wa dezo zimekwisha,’’ alisema Rage.
Alisema kwamba anachokifanya kwa wakati huu ni
kuweka mazingira mazuri katika klabu hiyo na wiki ijayo ataitisha
mkutano wa katiba.
Rage aliingia madarakani Mei, 2010 kwa kura 785
akimbwaga, Hassan Hassanol aliyepata kura 435. Kwa mujibu wa Katiba ya
Simba, uchaguzi mkuu ujao unatakiwa ufanyike Mei, 2014.
No comments:
Post a Comment