BABA YAKE DIAMOND PLATINUMZ AFURAHIA UAMUZI WA MWANAE KURUDIANA NA WEMA ASEMA PENNY HANA NYOTA YA KUWA NA MWANAE..!!
Baba mzazi wa Diamond, Abdul Jumaa
Akizungumza na mwanahabari wetu juzikati, Baba Diamond alisema
alifurahishwa mno na hatua ya mwanaye kurudiana na Wema kwani ndiye
mwanamke anayejielewa na ana nyota kali tofauti na warembo wengine
aliowahi kuwa nao.
“Wema ni mwanamke mwenye nyota kali sana na anapendwa na wengi. Siyo kama hao akina sijui Penny (Penniel Mungilwa).
“Hana majivuno hata mimi nilisema mwanzoni walipoachana kuwa Diamond
alipoteza bahati lakini sasa naamini atafika mbali zaidi kwani kama siyo
kuachana kwao, Diamond angekuwa mbali,” alisema.
Hata hivyo, alimtaka Diamond kutulia na Wema kwani ndiye mwanamke
sahihi kwake na aepuke kutangatanga kwani atashindwa kufanya mambo ya
maana yatakayomuwezesha kuwa juu zaidi ya hapo alipo kwa sasa.
Hivi karibuni Diamond alithibitisha kurudiana na Wema wakiwa China
lakini alipotua Bongo akaendelea na uhusiano wake na Penny hivyo
kuwaacha mashabiki wake njiapanda.
No comments:
Post a Comment