MECHI ya Simba na Yanga ilikuwa presha tupu kwani zaidi ya
mashabiki 20 wa timu hizo mbili wengi wao wakiwa wanawake, walizimia
kwenye mchezo huo uliochezwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam na matokeo kuwa sare ya 3-3.
Kitu cha kushangaza zaidi, shabiki namba moja wa
kike wa Yanga anayetambulika zaidi kwa jina moja la Mwantumu (Mama
Yanga) alizimia na kupandisha morali na kugalagala chini lakini pia
shabiki mmoja aling’atwa na mbwa.
Mwantumu alilazwa chini na alizungukwa na
mashabiki na viongozi mbalimbali wa Yanga mahali lilipo lango la
kuingilia wachezaji vyumbani upande wa Yanga kabla ya kupelekwa kwenye
vyumba vya huduma ya kwanza.
Walipofika watu wa huduma ya kwanza akiwa chini
ili kumpeleka chumbani, kiongozi mmoja ambaye alikuwa na Mwantumu
alisema: “Pamoja na matatizo hayo bado ana morali sana.”
Mbali na Mwantumu, Uwanja wa Taifa ulibadilika
kwani badala ya kuangalia mpira walishangaa watu wa huduma ya kwanza
walivyokuwa wanahangaika kuokoa watu.
Ilishangaza zaidi, wakati Yanga inaongoza mabao
matatu ambayo yalifungwa kipindi cha kwanza, mashabiki wa Yanga ndiyo
waliozimia zaidi na baadaye Simba walipoanza kuchomoa wao pia ndiyo
walianza kuzimia.
Ilikuwa maajabu, Yanga walipokuwa wanafunga mabao
ndio mashabiki wao wengi walivyokuwa wanazimia. Simba walipoanza
kurudisha mabao ndivyo mashabiki wao wengi wakaanza kuzirai. Haijawahi
kutokea.
Kiongozi wa kikosi cha maafa wa Msalaba Mwekundu,
Bashiri Mgamba baada ya mechi alisema mashabiki zaidi ya 20 walikuwa
wamezimia.
Ingawa idadi hiyo aliyoitaja iliongezeka zaidi kwani watu walizidi kuzimia hata baada ya mchezo
No comments:
Post a Comment