Kamishna
wa Elimu Profesa Eustella Bhalalusesa ameliambia gazeti la Habari Leo
kuwa Serikali itabadili mfumo wa upangaji alama za ufaulu wa mitihani ya
Sekondari ili kazi anazofanya mwanafunzi shuleni, zitumike katika
kumpatia alama ya ufaulu katika mtihani wa mwisho, mfumo unaolandana na
ule unaotumika katika Vyuo Vikuu..
Tayari Serikali imetuma dokezo, ambalo lipo katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa wadau wa elimu ili kupata maoni yao kabla ya kuanzisha mfumo huo.
Tayari Serikali imetuma dokezo, ambalo lipo katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa wadau wa elimu ili kupata maoni yao kabla ya kuanzisha mfumo huo.
Dodoso hilo limeeleza kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi zitachangia asilimia hamsini na mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini pia.
Mathalani, kwa mtihani wenye alama za jumla ya 100, mwanafunzi akipata alama 50 kupitia kazi za shule, atatakiwa kutafuta alama 50 katika mtihani wa mwisho.
Kwa kutumia mfumo huu, mwanafunzi atakuwa anakwenda kufanya mtihani akiwa tayari anajua alama za mchango wa kazi shuleni (continuous assessment) na kuwa na hakika ya anachotakiwa kukipata wakati anakwenda kufanya katika mtihani:
“Hatutaki kuona mwanafunzi hanufaiki na kile alichokivuna akiwa shule. Mfano mfumo wa sasa mwanafunzi aliyepata alama F ni aliyepata alama kati ya 0-34.
"Lakini hapo kuna wanafunzi ambao wamezidiana kwa mfano aliyepata alama 20, hawezi kuwa sawa na aliyepata 0 ingawa wote wanawekwa kundi la F,” alifafanua Profesa Bhalalusesa.
“Hata hivyo, kumekuwa na mitizamo na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi. Mfumo huu hata hivyo hautumiki kwa wanafunzi wa kujitegemea,” lilieleza dokezo hilo.
-Habarileo
No comments:
Post a Comment