Manchester, England. Kocha wa zamani wa
Manchester United, Alex Ferguson amesema atampa ushirikiano wa kutosha
kocha wa sasa wa Manchester United, David Moyes.
Ferguson alisema hayo wakati alipokuwa akizindua
kitabu chake ambacho kimewakosoa nyota wengi aliokuwa nao Manchester
United kama Roy Keane, David Beckham, Wayne Rooney, Carlos Tevez na
Anderson.
“Mimi nilipojiunga Manchester United nilipewa
ushirikiano wa kutosha na Matt Busby, alinisaidia sana, ninatarajia
kumsaidia David Moyes kama mimi nilivyosaidiwa na Busby,” alisema
Ferguson.
Kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu msimu huu kocha Moyes
alisema ratiba siyo nzuri kwa upande wa Man U kwani katika mechi zake
tano za mwanzo ilipangiwa kucheza na Chelsea, Liverpool na Manchester
City. Akizungumzia hilo kocha Ferguson alisema,”hata mimi nilipoiona
ratiba ya msimu huu niliona Manchester itakuwa na wakati mgumu mwanzoni
mwa msimu.”
Alisema,”Hata hivyo watu wengi wanasahau Man U ni timu ambayo inaweza kutoka chini na kupanda mpaka juu na kutwaa ubingwa.”
No comments:
Post a Comment