STRAIKA Mtanzania anayeichezea TP Mazembe, Mbwana Samatta, ana mechi mbili tu za kuthibitisha ubora wa upachikaji mabao Afrika ingawa kuna wachezaji; Vincent Die Foneye wa ENPPI (Misri) na Sonito wa Liga Muculmana (Msumbiji) wanaomsumbua akili kwa mabao yao sita.
Hata hivyo Samatta anaweza kuwapiku wanasoka hao kwa vile timu zao zimeshatolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mazembe inacheza fainali ya nyumbani na ugenini
dhidi ya CS Sfaxien Tunisia kwenye michuano hiyo. Mechi ya kwanza
itachezwa kati ya Novemba 22 na 24 na marudiano itakuwa Novemba 29 na
Desemba Mosi.
Samatta ana mabao matano sawa na Idrissa Kouyate
wa CS Sfaxien na Sassi wa Etoile Sahel ya Tunisia, wote hao wana nafasi
ya kutwaa zawadi ya Mfungaji Bora.
No comments:
Post a Comment