Viwanja hivyo vinauzwa kwa bei ya kuanzia Sh10 milioni na kuendelea .
Dar es Salaam. Taasisi ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania, (UTT) imeanza kuuza viwanja kwa wananchi katika eneo la Mapinga wilayani Bagamoyo.
Lengo ni kurahisisha maendeleo kwa wananchi kwa
kuwa na viwanja bora vilivyounganishwa na miundombinu ya maji, umeme na
barabara. Pia kuongeza thamani ya mji wa Bagamoyo unaotarajia kuwa na
bandari Msanifu Mwandamizi wa mradi huo kutoka UTT, Godfrey Mwakabole
,alisema katika mradi wa kwanza viwanja 246 ambavyo vimepimwa na
kuwekewa huduma zote muhimu za barabara, maji na umeme vitauzwa kwa
wananchi.
Mwakabole aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa mpango wa uuzaji wa viwanja hivyo.
“Eneo zima la mradi huu wa Mapinga lina viwanja
1,000 na UTT tayari tumesha anza kuuza viwanja 246 na awamu ya pili ya
mradi huu itakuwa ya kujenga nyumba ambazo zitauza kwa bei
nafuu,”alisema Makabole.
Alisema kiwanja cha bei ya nchini kitakuwa Sh10 milion na kwamba mradi wa kwanza utakamilika mwaka 2015.
Ofisa Mkuu wa Usimamizi wa mradi, Shakiru
Abdulkarimu alisema UTT inashirikiana na manispaa katika upimaji wa
viwanja katika maeneo mbalimbali.
Alisema tayari Manispaa ya Bukoba imeshapima viwanja 5000 na upimaji wa viwanja kama huo unaendelea Lindi na Mtwara.
No comments:
Post a Comment