MAPIGANO DHIDI YA WAASI WA M23 HUKO CONGO YAPAMBA MOTO
Mapigano
mapya yamezuka jana Jumamosi(26.10.2013) kati ya majeshi ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo na waasi katika siku ya pili ya machafuko ambayo
yamesababisha miito ya utulivu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa .
Mapigano
ya hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yamezuka
siku ya Ijumaa, chini ya wiki moja baada ya serikali mjini Kinshasa na
waasi wa kundi la M23 kutangaza kuwa mazungumzo ya amani mjini Kampala
yamevunjika.
Jeshi
la serikali jioni ya Jumamosi lilisema kuwa limeukamata mji wa Kibumba ,
mji ulioko kilometa 25 kaskazini ya eneo mji wa mashariki mwa nchi hiyo
wa Goma ambao unatoa njia kuelekea katika eneo la waasi upande wa
kaskazini.
"Kibumba
uko chini ya udhibiti wa jeshi la serikali FARDC kuanzia leo," afisa
mwandamizi wa jeshi ameliambia shirika la habari la AFP mjini Goma.
Waasi hawakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia tamko hilo.
Upande
mwingine wa mapigano umeanza ghasia siku ya Jumamosi wakati jeshi
liliposhambulia maeneo ya kundi la M23 katika jimbo la Mabenga, kiasi ya
kilometa 80 kaskazini mwa goma na karibu na mpaka na Uganda.(P.T)
Jeshi
"limeanzisha mashambulizi katika barabara ya Mabenga kuelekea Kahunga.
Linatumia wanajeshi, vifaru na makombora", afisa mwingine wa jeshi
amesema, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina.
Waasi wamethibitisha kuwa mapigano yamesambaa hadi katika eneo la kaskazini.
Mapigano yasambaa
"Mapigano yanaongezeka katika maeneo yote," kiongozi wa kisiasa wa M23 Bertrand Bisimwa amesema katika tovuti ya kundi hilo.
Mjumbe
maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika mzozo huo,
Mary Robinson na Martin Kobler, wametoa taarifa wakielezea wasi wasi
wao mkubwa kuhusiana na mapigano hayo mapya.
"Tunatoa
wito kwa pande zote kuonyesha hali ya uvumilivu na kuanza tena
majadiliano mjini Kampala," wamesema. Marekani imesema kuwa imesitushwa
na ripoti za kuongezeka kwa mapigano, licha ya miito ya kimataifa kwa
pande hizo kuonesha hali ya kuvumiliana.
"Tunawasi
wasi mkubwa juu ya ripoti za mapigano ya mpakani, " katika jimbo la
Kivu ya kaskazini, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Jen Psaki
amesema katika taarifa, akizitaka pande zinazopigana, "kuacha vitendo
vitakavyozidisha hali hiyo".
Taarifa
ya Psaki imezitaka pande hizo kurejea katika majadiliano, " ili kuondoa
vikwazo vilivyobaki kuelekea kutiwa saini kwa makubaliano ya mwisho, na
ya msingi, ambayo yataleta usitishaji wa kudumu wa mapigano na
kuwawajibisha wake ambao wamefanya uhalifu mkubwa".
Jumuiya ya kimataifa yaonya
Mkuu
wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton pia
ametoa wito, "kwa wahusika wote katika eneo hilo kuzuwia kuongezeka
zaidi kwa hali hiyo na kuufanya mzozo huo wa kimataifa".
Athari
zilizoripotiwa ndani ya mpaka wa Rwanda kutokana na matukio ya hivi
karibuni yanapaswa kufanyiwa uchunguzi kwa pamoja," amesema Ashton.
Waasi
wanadai kuwa jeshi la serikali lilishambulia maeneo yao mapema siku ya
Ijumaa, lakini jeshi la serikali linasisitiza kuwa lilishambuliwa
kwanza, madai ambayo yanaungwa mkono na duru kutoka ujumbe wa kulinda
amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO.
Wakati
huo huo jeshi la serikali ya Congo limesema limepata mafanikio makubwa
dhidi ya waasi wa M23 katika siku ya pili ya mapigano makali jana
Jumamosi na kuitaka nchi jirani ya Rwanda kusaidia kuwanyang'anya silaha
waasi.
No comments:
Post a Comment