Waziri Mkuu,Mizengo Pinda amewaonya baadhi ya Watanzania
wanaokuja katika Jiji la Guangzhou nchini China kwa ajili ya kununua
bidhaa mbalimbali,waache kuuza hati zao za kusafiria kwa raia wa nchi
nyingine kama njia ya kujiongeza kipato. Alitoa onyo hilo jana usiku
wakati akizungumza na Watanzania wanaofanya biashara na wale wanaoishi
katika Jiji la Guangzhou, jimbo la Guangdong ambalo ni jiji kubwa la
biashara lililoko kusini mwa China.
Alisema wengi wa wafanyabiashara hao wanapouza
pasipoti zao wanasingizia kuwa zimepotea ndio maana kuna malalamiko
mengi kutoka kwa Watanzania wanaofika katika jimbo hilo kudai wanaibiwa
hati zao za kusafiria wakati sio kweli.
Wakati wa mazungumzo hayo, mmoja wa Watanzania
aliyejitambulisha kwa jina la Ambrose Lugai alisema changamoto nyingi
zinazowakabili Watanzania waishio katika jimbo hilo na moja ya tatizo
hilo ni kuibiwa kwa hati za kusafiria za Watanzania.
Lugai alisema tatizo la wafanyabiashara wengi
kupoteza pasipoti limekuwa sugu na kila siku linaongezeka na cha ajabu
linawatokea wafanyabiashara wa kutoka Tanzania tu.
Alimwomba Waziri Mkuu awasaidie kuzungumza na
Serikali ya jimbo hilo ili Watanzania wawe wanaacha pasipoti hotelini
wakati wanapoenda mitaani, badala yake wapewe karatasi nyingine ya
kuwatambulisha mitaani.
Akijibu hoja hiyo ya Lugai, Waziri Mkuu alisema
suala hilo linamshangaza kwamba inakuwaje hati za wafanyabiashara wa
Tanzania tu ndio zinaibiwa wakati wafanyabiashara wanaofika kwenye jimbo
hilo ni wengi
No comments:
Post a Comment