Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa akizungumzia kuhusiana na tukio la mtoto wa miaka 11 aliyeolewa na binamu yake. Mtoto huyo sasa anaishi nyumbani kwake. Picha na Sharon Sauwa.
Imetokea Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa amchukua mtoto huyo aliyeolewa, aahidi kumsomesha.
Dodoma. Katika
hali ya kawaida, binti wa miaka 11 (jina linahifadhiwa kwa sababu za
kimaadili), mkazi wa kijiji cha Kongogo, Wilayani Bahi mkoani Dodoma
hivi karibuni aliolewa na binamu yake, kisha ndoa yake kuvunjwa na
Serikali.
Hakuna taarifa nyingi za mabinti kuolewa katika
umri mdogo katika wilaya hiyo mbali ya kuwepo kwa watoto wadogo ambao
huondolewa katika masomo na wengine kushindwa kupata elimu kwa sababu
wazazi wao huwapeleka migodini na wengine maeneo ya mijini kutumikishwa
majumbani.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa,
anasema wilaya yake inaongoza mkoani hapa kwa kuwa na kiwango kikubwa
cha vitendo vya ukeketaji wa wanawake ikiwa nayo ni sehemu ya ukatili
wa kijinsia.
Lakini kwa tukio hilo, lililojitokeza katika moja
ya familia ya wafugaji, kunaweza kukafanya umuhimu wa kujikita katika
utafiti wa kina kuliangalia suala la kuolewa katika umri mdogo lina
ukubwa gani mkoani hapa.
“Hazungumzi na mtu yeyote humu ndani na unaweza
kumsemesha anakuangalia tu, ila anazungumza na mimi (Mkwasa), ama
wasichana wawili tu wa hapa ndani ambao anashinda nao,”anasema Mkwasa
ambaye sasa anamlea mtoto huyo.
Maneno hayo yanathibitishwa na mwandishi wa makala
haya, aliyefika nyumbani kwa Mkwasa kwa nia ya kuzungumza naye baada
ya kupata taarifa ya kuwepo kwa mtoto huyo.
Anapoitwa kwa nia ya kutambulishwa, anafika
mlangoni na kubaki akiangalia tu huku wakati mwingine akiinamisha macho
yake chini na hata anaposalimiwa haitikii, badala yake anaondoka na
kwenda kujificha ndani.
Hali hii iliweka ugumu katika kufanya mahojiano
naye, lakini kwa usiri mkubwa inatubidi kumtumia mmoja wa wasichana
ambaye amekuwa muwazi kwake kusikia nini kilichotokea.
Si kwamba hazungumzi, la hasha binti huyu ni
mzungumzaji mzuri na tunapotoka nje na kuwaacha wawili ndani ya sebule
hiyo tunawasikia wakizungumza na hata kucheka kwa sauti.
Mkwasa anasema siku za mwanzoni binti huyo
alikuwa haongei na mtu yoyote lakini baada ya kuhudumiwa na
mwanasaikolojia ambaye hufika nyumbani kwake kila baada ya siku tatu,
alianza kuongea.
Akisimulia tukio hilo, Mkwasa anasema mtoto huyo
alikutwa akizubaa na akiwa amechoka katika kijiji cha Mindola baada ya
kutoroka kwa mwanamume aliyeolewa naye.
No comments:
Post a Comment