BAADHI ya wanachama wa matawi ya Klabu ya Simba wamewaonya watu ambao
wanauza bidhaa zenye nembo ya timu hiyo katika pambano lake na Coastal
Union lililofanyika juzi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa.
Onyo hilo walilitoa kwa kuandika bango ambalo waliliweka kwenye lango kuu la kuingilia magari ambalo lilisomeka: “Ni marufuku kwa wauzaji wa jezi kuuza jezi feki za timu ya Simba au bidhaa zenye nembo ya Simba kwenye mechi dhidi ya Coastal, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayebainika.”
Akizungumza na Championi Ijumaa, mmoja wa wanachama wa timu hiyo aliyejitambulisha kwa jina la John Lucas kutoka Tawi la Mpira Pesa, alisema kuwa kuna watu wanajinufaisha kwa kuuza bidhaa feki za timu hiyo.
“Kuna wafanyabiashara ambao si waaminifu ambao wanauza bidhaa feki za timu yetu na kujinufaisha wao, ndiyo maana tumetoa tangazo hili,” alisema.

No comments:
Post a Comment