BAADHI ya madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara,
wamegomea agizo la mkuu wa mkoa huo kwenye kikao cha baraza.
Madiwani hao wamekataa kusoma taarifa za utekelezaji wa miradi ya
maendeleo mbele ya kikao cha baraza, wakidai kuwa jambo hilo linafanywa
katika vikao vya kata na hawana sababu ya kufanya hivyo.
Walieleza kuwa pamoja na kwamba agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa
wao, hawako tayari kulifuata kwani hawajawahi kukaa na kujadili kuhusu
watendaji wa kata kuingia kwenye mabaraza na kusoma taarifa kwa niaba
yao.
“Haya mambo yanafanyika kule kwenye kata, hivyo sisi hatuwezi kusomewa
taarifa za kata zetu na watendaji, kama wanataka hao watendaji wasome
wao kama wao lakini sisi wasitushirikishe,” alisema John Farayo, Diwani
wa Endashwod.
Hata hivyo, madiwani hao walisema kuwa mpango ulioanzishwa na mkuu wa
mkoa sio mbaya ila viongozi wa halmashauri hiyo hawakutoa nafasi kwao
kujadili muhtasari ulioletwa na mkuu huyo badala yake wameamua kuanzisha
ghafla.
“Hatuna kanuni ya mwaka 2013 kama ilivyo taarifa na waraka wa mkuu wa mkoa na baraza la madiwani.
“Ni mamlaka hivyo hakuna zaidi yake, hivyo wajumbe wameona hawana mtu
wa kumsomea taarifa hii,” aliongeza Masala Bajuta, Diwani wa
Gisambalang’.
Agizo la kusoma taarifa za utekelezaji wa maendeleo lilitolewa na mkuu
wa mkoa huu, Elaston Mbwilo, kwenye baraza maalumu la madiwani kusomewa
taarifa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
lililofanyika Oktoba 7, mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment