Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa) limetangaza viwango vipya vya
ubora wa soka kwa Oktoba, huku Tanzania ikiporomoka kwa nafasi mbili
kutoka ile ya 128 hadi 130.
Licha ya kuporomoka, pia Tanzania imejikuta
ikikamata mkia kwa ubora wa soka miongoni mwa nchi tano za Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, Uganda imeteremka kwa
nafasi nne kutoka 81 hadi 85, hata hivyo imeendelea kushikilia rekodi ya
nchi inayoongoza kwa ubora kati ya nchi tano za Afrika Mashariki.
Nchi nyingine zinazounda jumuiya hiyo na viwango
vyao vya ubora ni Ethiopia iliyoshuka kwa nafasi mbili kutoka 93 hadi
95, Kenya nafasi ya 118, wakati Burundi imepanda kwa nafasi mbili kutoka
120 hadi 122 na Rwanda ambayo pia imechupa kwa nafasi mbili kutoka 129
hadi 131.
Ivory Coast imeendelea kukaa kileleni ikishikilia
nafasi ya kwanza kwa ubora wa soka Afrika, huku ikipaa kwa nafasi mbili
kutoka 19 hadi 17, wakati mabingwa wa Afrika, Nigeria wakiwa
wamejitutumua na kupanda kwa nafasi tatu kutoka 36 hadi 33.
No comments:
Post a Comment