Monday, 21 October 2013

WAZIRI WA JK AFANYA KIOJA JIMBONI KWAKE

Waziri Tibaijuka atoa kali jimboni; atembea na sufuria ya Pilau kushawishi wananchi kuhudhria Mkutano

Katika hali isiyo ya kawaida Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitinga kwenye viwanja vya mkutano na masufuria ya Pliau. Mwanzoni wananchi wa Kijiji cha Kiga Kata Rulalnda Jimbo la Muleba Kusini waliona kama ni maagizo pale Waziri alipotinga eneo la mkutano akiwa na magari matatu na mojawapo likiwa ni gari aina ya Canter likiwa limejaa sufuria zenye Pilau kama gia ya kushawishi watu wajae kwenye mkutano ule.

Kiroja hiki cha karne kiliwaacha wananchi midomo wazi huku wengine wakijiuliza kama Waziri alikuwa amefika kule kuhani msiba, kula matanga, kufanya matambiko au kufanya mkutano? Wananchi wengine walisikika wakisema Waziri atakuwa anafanya mambo ya kishirikina pasipo wananchi kujua, huku wengine wakijiuliza mazingira yaliyopikiwa chakula kile na wengine wakienda mbali zaidi kujiuliza kama chakula kile kilikuwa na baraka za Mkemia Mkuu wa Serikali.

Mimi baada ya kupata ujumbe mfupi (sms) kutoka kwa Kamanda aishie Dar na kunipa kazi ya kufuatilia kuona kama kweli Pilau lilikuwa likigawiwa pale Kiga eneo la Mkutano niliondoka na Pikipiki na kufanilkiwa kufika eneo la tukio. Ama kweli masufuria yalikuwa yamejaa, kwa haraka haraka niliona sufuria sita, mabox ya soda huku wakinamama wakiimba kwa shangwe. Umaskini uliniweka kwenye mazingira magumu muda ule maana ningelikuwa na simu ya Kamera ningepiga picha pamoja na kwamba kulikuwepo ulinzi wa mgambo kuhakikisha mambo hayatokei.
Hii ndiyo story ya leo hapa mjini Muleba na Maeneo ya Bomani.
Wananchi wanajuuliza maswali mengi kuhusu hii stahili mpya ya Waziri;

1. Je Waziri keshajua kwamba wananchi hawawezi kuhudhria mikutano yake na sasa anakuja na kichocheo?
2. Ni kweli waziri anao uwezo wa kutembea na masufuria ya pilau jimbo zima kila anatakapofanya mikutano?
3. Je huu ndo utekerezaji wa ahadi alizoahidi wananchi wakati wa kampeni 2010?
4. Je chakula cha siku moja na penyewe mlo mmoja unawapunguziaje wananchi na wakazi wa Kiga makali ya maisha waliyonayo?
5. Je ni kweli Waziri ameshatambua kwamba hakubaliki Jimboni kwake na ndani ya Chama chake kwamba si mtu sahihi wa kuwaongoza wana Muleba?
6. Je tutatajie kitu gani mbele hasa baada ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kuzidi kuchanua Jimboni kwake? Niliwahi kusema wiki chache zilizopita kwamba kuna bwana mdogo anaitwa Kashasira anamburuza sana Jimboni. Je hili ndo anguko la Profesa na CCM?
7. Kama wananchi waliahidiwa Umeme, Barabara, Maji safi, huduma bora za jamii hasa afya na elimu; kwa stahili hii wananchi watapata majibu ya ahadi hizo lini kama ameanza kutoka kwa stahili ya Pilau?

Kingine nilichoona ni wamama waliojichokea na wazee wengine wakicheza ngoma na kama kawaida ya wanaCCM, Waziri akawaahidi wakina mama shilingi 500,000 vikundi viwili ikiwa na maana shilingi 250,000 kila kikundi na wakina baba waliomchezea ngoma wakaahidiwa shilingi 500,000. Waziri Anna aliendelea kumimina ahadi nyingine mpya wakati za 2010 hajatekeleza kata moja.

Kuonyesha kwamba kuna mpasuko ndani ya CCM Muleba mama alikuwa mwenyewe bila hata Diwani wa eneo hilo bwana EVAT ERENEST maarufu kama Nduli Idd Amini Dada ambaye pia ni Katibu Mwnenezi wa CCM Wilaya. Zaidi hapakuwepo hata kiongozi mmoja wa CCM ngazi ya Wilaya. Wanabodi mzidi kutombea maana baada ya mapilau haya kitafuatia nini.

No comments:

Post a Comment