KIUNGO wa Manchester City, Yaya Toure, amealikwa kukutana na
bosi wa kitengo cha kuzuia ubaguzi wa rangi cha Shirikisho la Kimataifa
la Soka (Fifa) baada ya kudokeza kwamba huenda wachezaji weusi wakagomea
kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 kutokana na ubaguzi wa
rangi kukithiri nchini Russia.
Toure analalamika kwamba alibaguliwa na mashabiki
katika pambano la Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya CSKA ya Russia Jumanne
iliyopita na huenda akawashawishi wachezaji weusi wasiende Russia
kucheza Kombe la Dunia katika fainali zitakazofanyika huko.
Jeffrey Webb, ambaye anaongoza kitengo hicho cha
kuzuia ubaguzi wa rangi, jana Jumapili alisafiri mpaka London, England
akitazamia kuonana na Toure mara baada ya kumalizika kwa pambano kati ya
City dhidi ya Chelsea.
“Naenda kwenye mechi kwa matumaini ya kupata
nafasi ya kuonana na Yaya. Nimeomba kuonana naye. Nataka kujua Yaya
alivyojisikia na kupata stori nzima,” alisema Webb ambaye pia ni Makamu
wa Rais wa Fifa.
No comments:
Post a Comment