KOCHA wa Simba Abdallah Kibadeni amelaumu kuwa kuna hujuma
imefanyika kwa wachezaji wake, wakati Mholanzi wa Yanga, Ernest Brandts
amesema wachezaji wake hawako kiprofesheno.
Kibadeni aliweka wazi kuwa Yanga isingeweza
kuwafunga mechi hiyo lakini kwa sababu kuna watu wamevamia kambi yake na
kuwadanganya wachezaji wakacheza chini ya kiwango.
“Nawajua wachezaji wangu, kiwango kile si chao,
hawakutaka kucheza ndiyo maana tulifungwa mabao yale matatu kipindi cha
kwanza. Kuna watu wanakuja kambini na kuwapandikiza maneno wachezaji na
hao waliopandikizwa maneno hawakucheza vile inavyopaswa kipindi cha
kwanza wakaruhusu mabao matatu ya haraka haraka,”alisema Kibadeni katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana Jumapili.
“Tulivyokwenda mapumziko, nilizungumza nao na
nikawaambia, mmeshawapa mabao matatu yanatosha, sasa chezeni
mpira,”alisema Kibadeni ambaye alienda mbali na kuwazungumzia kiungo,
Abdulhalim Humoud ‘Gaucho’ na winga, Haruni Chanongo ambao aliwatoa na
kuwaingia, Said Ndemla na William ‘Gallas’.
“Siwezi kuwataja kwa majina, watajijua na
kujichuja wenyewe. Yule Humoud nilimpanga kwa makusudi kama mlivyoona
ndiyo maana nilimtoa,”alisema Kibadeni ambaye wiki iliyopita alikuwa
akilalamika kwamba kuna wachezaji ndani ya Simba ambao wanamtengenezea
majungu kwavile anawaambia ukweli na hawataki kufuata utaratibu wa kambi
yake.
Kocha wa Yanga, Mholanzi Ernest Brandts alisema:
“Tulistahili kushinda na ninachowalaumu wachezaji wangu hawako
kiprofesheno kwa sababu baada ya kushinda mabao 3-0 kwenye mapumziko
waliingia wanashangilia wakati mechi inaendelea. Nilishangaa sana.
“Wakati wa mapumziko walivyoingia kwenye vyumbani
walikuwa wanashangilia kama wameshinda mchezo, mpaka nikashangaa, sare
wameitaka wenyewe, tulipata nafasi nyingi na tukashindwa kuzitumia. Timu
nzima ilikuwa na upungufu, Luhende na Chuji walifanya makosa mawili
yakatugharimu,”alisisitiza Brandts.
Na alipoulizwa kama kuna hujuma, Brandts alisema
inawezekana. “Haiwezekani tuongoze mabao matatu na baadaye warudishe
yote, haiwezekani wachezaji wametuhujumu na kinachotakiwa tuwachomoe
baadhi yao,”alisikika shabiki mmoja maarufu.
No comments:
Post a Comment