Monday 9 December 2013

Balotelli atetea kiwango chake


STRAIKA Mario Balotelli amesema kilichokuwa kinazungumzwa juu yake ni kwa sababu alikuwa hafungi mabao, lakini ukweli halisi bado kiwango cha soka lake kipo juu.
Nyota huyo Mtaliano juzi Jumamosi alifunga mara mbili kwenye sare ya mabao 2-2 dhidi ya Livorno katika mchezo wa Ligi Kuu Italia maarufu Serie A.
Kaka alitengeneza bao la kwanza, kabla ya fowadi huyo wa zamani wa Manchester City kufunga kwa mpira wa adhabu katika dakika 83 na kuisawazishia Rossoneri.
“Hivi ndivyo soka ilivyo. Wakati mwingine mpira utazama golini,” alisema Balotelli akizungumzia mpira wake uliogonga mwamba ambao ungeweza kuitoa kimasomaso AC Milan.
“Siku zote nimekuwa fiti, sina tatizo lolote na vitu vinavyoandikwa. Kilichokosekana ni kwamba nilikuwa sifungi tu.”
Balotelli alisema AC Milan kwa sasa wapo kwenye presha kubwa baada ya kuwa nyuma kwa pointi 22 dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Juventus.

No comments:

Post a Comment