Thursday 19 December 2013

FIFA YATOA RUKSA OKWI KUKIPIGA YANGA!

Hatimaye shirikisho la soka duniani FIFA, limeidhinisha rasmi uhamisho mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Anorld Okwi kusajiliwa na mabingwa wa Tanzania, Young Africans katika mechi zake za mashindano.
Akizungumza na MTN Football, Kaimu Mkurugenzi wa mashindano wa FUFA, Decolas Kiiza amesema mchezaji huyo sasa ni ruksa kwenda Tanzania.
"Mapema wiki hii tuliiandikia barua FIFA watupe ufafanuzi zaidi kama ni sahihi Okwi kuhamia katika klabu ya Tanzania, na sasa wametujibu kwamba mchezaji huyo yuko huru kuhamia kokote" alisema Kiiza

No comments:

Post a Comment