Thursday 19 December 2013

HIZI NDIZO SABABU ZINAZOSABABISHA WANAWAKE WENGI KUTOFIKA KILELENI WAKATI WA TENDO LA NDOA...

Wanawake wengi nchini na duniani kwa ujumla wanasumbuliwa na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa ( LACK OF LIBIDO ) pamoja na tatizo la kutofika kileleni. Sababu zinazo changia tatizo hili zimegawanyika katika makundi makuu mawili : ( A ) Sababu za Kisaikolojia { Psychological ) na ( B ) Sababu za Kimwili { Physical }

A. SABABU ZA KIMWILI " PHYSICAL"


1. Anaemia ( ugonjwa huu ni very common kwa wanawake kwa sababu ya kupoteza madini ya chuma wakati wa hedhi )

2. Ulevi Kupita kiasi ( Alcoholism )
3. Utumiaji wa Dawa Za Kulevya ( Kama Vile bangi n.k )
4. Magonjwa makubwa kama vile kisukari.

( Sababu zipo nyingi sana, hizi ni baadhi tu )

B : SABABU ZA KISAIKOLOJIA " PSYCHOLOGICAL "

1. Depression
2. Stress and overwork
3Anxiety " Woga"
4. Kunyanyaswa kijinsia ama kubakwa wakati wa utotoni
5 Kuwa katika matatizo makubwa na mpenzi wako.
6. Kuishi katika mazingira magumu mfano kushare nyumba ama chumba na wazazi wako, wakwe zako ama watoto wako.

HIZI NI BAADHI YA SABABU ZINAZO WAFANYA WANAWAKE WENGI LEO HII KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA NA KUTOFURAHIA TENDO HILO.
Hata hivyo sababu hizi hazimuhusu kila mwanamke, wanawake wengine wanasumbuliwa na tatizo hilo tangu walipo vunja ungo.

KUSHINDWA KUFIKA KILELENI KWA WANAWAKE : 
Hali hii husababishwa na sababu nyingi za kimwili na kisaikolojia kama vile kuwa na msongo wa mawazo, presha,woga, wasiwasi wa tendo la ndoa ,kubakwa ama kudhalilishwa wakati wa utotoni, na/ama kufanya tendo hilo na mwanaume mwenye uwezo mdogo wa kiufundi.

No comments:

Post a Comment